Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija amepokea jumla ya madawati 353, viti 3 vya kutembelea watoto wenye ulemavu, mipira 50 pamoja na tanki la kuhifadhia maji kutoka Doris Mollel Foundation pamoja na KCA kwaajili ya shule ya msingi Kakora yakilenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi katika shule hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo Februari 28,2026, Mhe. Ludigija ametoa shukrani za dhati kwa taasisi hizo kwa moyo wa kujitolea na kuona umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya elimu.
Amesema upatikanaji wa madawati na vifaa vingine utasaidia kupunguza changamoto kwa wanafunzi hivyo kuongeza ari ya kujifunza.
“Napenda kuishukuru sana Doris Mollel Foundation na KCA kwa msaada huu mkubwa wa madawati 353 pamoja na vifaa vingine Hii ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wetu na kuongeza ufaulu wao kitaaluma,” alisema Mhe. Ludigija.
Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu, akisisitiza kuwa jukumu la kuijenga jamii ni la pamoja.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Doris Mollel Foundation Bi.Doris Mollel amesema kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia sekta za kijamii ikiwemo elimu na afya, ili kuhakikisha watoto wanapata fursa bora ya kufikia ndoto zao.
Wananchi pamoja na walimu wameshukuru msaada huo ambao utaleta mabadiliko chanya katika shule hiyo na utaongeza na kuwa chachu kwa wanafunzi kupenda masomo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.