MILIONI 246 YATOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU
Posted on: March 3rd, 2026
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amekabidhi milioni 246 kwa vikundi 11 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Ludigija amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuona mikopo hii inabadirisha maisha yao kiuchumi kwa kutumia fedha hizi kuzalisha ili kuboresha maisha.
Vilevile amewataka kwenda kufanya shughuli walizoandika kwenye andiko mradi siyo kwenda kugawana na kufanya vitu visivyohusika
" kumbukeni huu ni mkopo usio na riba na nendeni mkafanyie kazi mlizoandika siyo kutumia fedha hizi kuoa, kushona suti na vitenge au shughuli yoyote isiyohusika"
Aidha amewataka walezi wa vikundi hivyo kuwa walezi siyo wamiliki wa vikundi " walezi fanyeni kazi yenu ya kulea siyo kwenda kumiliki kikundi na kusababisha vikundi kuyumba na hili tutalifuatilia" Ludigija
Katika hafla hiyo ameshiriki Mwenyeki wa Halmashauri Mhe. Lameck Hole ambaye amesema Halmashauri inaendelea kutenga fedha kwaajili ya mikopo inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri, pia amewahimiza kurudisha mkopo huo kwa wakati ili waweze kupewa watu wengine
" niwaombe sana mjitahidi kutumie fedha hizi kwa kuzalisha na Serikali inataka fedha ikufikie wewe na imfikie mtu mwingine kwahiyo kazitumieni kwa malengo yaliyokusudiwa"
Kaimu Mkurugenzi Bi. Ndelisho Moshi amevitaka vikundi hivyo kwenda kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili lengo la fedha hiyo litimie.
Wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru Serikali kwa kuendeleza utaratibu huo wa kutoa mikopo ili kuinua maisha ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu
" tunaishukuru Serikali hii mikopo imetusaidia tulianza na mkopo wa milioni 30 tukarejesha sasa hivi tumepewa milioni 96 ambazo zinakwenda kuinua biashara yetu ambapo tunajishughulisha na kutengeneza samani mbalimbali" amesema Kenedy Stephano Mwenyekiti kikundi cha vijana Fundi Seleman