Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba Ndug Mohamed Ngesinda amewataka wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi ya Kata,vijiji na Wilaya kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa uaminifu.
Ameyasema hayo leo Septemba 30,2024 wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi hao ambao wameapa kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa.
" baada ya mafunzo haya tunatarajia kuwa mtafanya kazi vizuri kwa weledi ili kuhakikisha shughuli za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinakamilika vizuri" amesema Ngesinda
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zimefundishwa ikiwa ni pamoja na usimamizi na utunzaji wa nyaraka za Uchaguzi, ujazaji wa fomu mbalimbali zinazohusiana na shughuli za uchaguzi.
Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt.Amon D Mkoga amewataka watumishi wote waliopangiwa kufanya kazi ngazi ya Kata na vijiji kwenda kutekeleza maelekezo yote na kuhakikisha uhamasishaji wa Wananchi kushiriki zoezi la kujiandikisha na kupiga kura unafanyika kila kitongoji.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika Novemba 27,2024 ambapo wananchi wote watakaojiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuanzia 11 Oktoba hadi 20 ,2024 ndio watakaoweza kupiga kura.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.