Waziri wa Viawanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga ( MB) amewataka COPLA, TMX na bodi ya usimamizi wa stakabadhi ghalani kuhakikisha wanashirikiana na mkulima kuanzia uzalishaji shambani hadi uuzwaji sokoni, ameyasema hayo leo 25 Feb,2026 kwenye ziara Wilayani Kwimba wakati akikagua mwenendo wa mnada wa choroko Hungumalwa.
Aidha amewataka wafanya biashara waelewe kuwa utaratibu wa sasa wa kuuza choroko ni kwa mfumo wa stakabadhi ghalani hivyo wametakiwa kuwa waaminifu na kujiepusha na utoroshaji
" haitakiwi na hairuhusiwi kutorosha kwa namna yoyote ile lazima tukubaliane na twende na utaratibu tuliojiwekea" amesema Kapinga
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija ameeleza kuwa mfumo huo umekuwa na matokeo chanya kwa mapato ya Halmashauri katika kuhakikisha mapato yanapatikana bila usumbufu
'Sisi kutokana na mfumo wa stakabadhi ghalani tunapata takwimu sahihi na hivyo kupata mapato ya Halmashauri kwa urahisi na kwa usahihi na tumejipanga kudhibiti utoroshaji.
Katika ziara hiyo ameshiriki Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Mosses Bujaga ambaye ameomba tozo zipungue ili wakulima wapate bei kubwa zaidi yenye kuwanufaisha" ni vizuri hizi tozo ziangaliwe vizuri kama inawezekana kupunguzwa ili wakulima wanufaike zaidi"
Naye Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Cosmas Bulala ametumia nafasi hiyo kumuomba waziri kuzitaka Taasisi zinazosimamia stakabadhi ghalani kushiriki kuanzia uzalishaji shambani hadi sokoni
"wakati tunalima hatumuoni TMX, WRB na COPLA muda wa kuvuna wanakuja tunaomba Taasisi hizi washiriki kuanzia uzalishaji shambani hadi kuvuna kwa kutoa mbolea,mbegu na ikiwezekana tuongeze tija ya kilimo kwa kuboresha kilimo hasa chenye pembejeo bora" amesema Bulala
Aidha Mkurugenzi wa bodi ya usimamizi wa stakabadhi ghalani Bwana Asangye Bangu amewahakikishia wakulima kuendelea kuboresha mfumo huo " katika utekelezaji wa stakabadhi ghalani hiki ulichokiona ni hatua kubwa sana ambapo sasa uuzaji kupitia stakabadhi ghalani umekubalika kwa wakulima wa Kwimba na sasa niwahakikishie kwamba wakulima sasa wanazifahamu bei na hawapati shida kuuza mazao yao"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.