• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Kushughulikia Malalamiko

HALMASHAURI YA WILAYA YA KWIMBA

UTARATIBU WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO SERIKALINI

UTANGULIZI

Serikali imekuwa ikitoa maelekezo ya namna ya kushugulikia malalamiko katika Taasisi za zake ikiwa ni pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Maelekezo hayo yamekuwa yakitolewa kwa njia ya mafunzo na nyaraka mbalimabli. Kipeperushi hiki kimetumia maelezo yaliyotolewa na Ofisi ya Rais Ikulu katika kikao cha kazi kwa Wakuu wa Idara ya Utawala na Utumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wataalam wa Sekretarieti za Mikoa kilichofanyika tarehe 14 -19 Desemba, 2009.

1.0 MAANA YA MALALAMIKO:

Malalamiko yanaweza kutafsiriwa kama maelezo au tamko la kuonyesha kutoridhika kuhusu jambo lolote. Kutoridhika huko kunaweza kuwa ni kuhusu uamuzi au utekelezaji wa suala fulani. Malalamiko yanaweza kusababisha ufanisi na ushirikiano hasa mahala pa kazi ukapungua hivyo kuleta athari za kiutendaji kazi.

1.2 WAKATI GANI MTEJA KATIKA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA ANAWEZA KUTOA MALALAMIKO:

Mteja katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa anaweza kutoa malalamiko yake pale ambapo ataona uamuzi ama utekelezaji wa jambo fulani siyo sahihi, siyo wa haki au ni kinyume cha Sheria na taratibu zilizowekwa.

1.3 UMUHIMU WA KUSIKILIZA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO:

Kusikiliza na kushughulikia malalamiko mahali popote ni muhimu kwasababu:

  1. Ni njia mojawapo ya kutumikia jamii na kutatua matatizo ya watumishi.
  2. Inasaidia kuwepo amani na utulivu katika jamii na mahala pa kazi.
  3. Inasaida kuwepo na ushirikiano mahala pa kazi hivyo kuleta utendaji mzuri mahala pa kazi.
  4. Ni njia nzuri ya kuelewa matatizo yanayowakabili watu.
  5. Vilevile inasaidia kuelewa kama kuna dosari katika mfumo wa uendeshaji au udhaifu wa watendaji wenyewe.

Hivyo, ni lazima kila mtendaji kwenye nafasi yake awajibike ipasavyo kuhakikisha malalamiko yanapungua. Haimaanishi kupunguza malalamiko kwa kuwakataa walalamikaji bali kwa kufanya yafautayo:-

  1. Kuzingatia Sheria na Taratibu wakati wote wa utendaji wa kazi.
  2. Kuwajibika na kutekeleza majukumu ipasavyo na kwa wakati muafaka.
  3. Kutenda haki kwa kila mtu wakati wote.
  4. Kuepuka upendeleo.
  5. Kutotenda uonevu..

2.0 UTARATIBU WA KUSHUGHUKILIA MALALAMIKO.

Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) inapokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mikoa na wananchi wa kawaida kuhusu masuala mbalimbali ambayo pengine yanahusiana na huduma wanazopaswa kupata toka Halmashauri, Mikoa, Ofisi nyingine za Serikali.

Malalamiko hayo huwasilishwa kwa njia zifuatazo:-

  1. Njia ya ana kwa ana.
  2. Kwa njia ya maandishi (barua) na masanduku ya maoni.
  3. Njia ya vyombo vya habari kama vile magazeti na luninga.

Mlalamikaji atatakiwa kutumia njia mojawapo kati ya zilizotajwa hapo juu na kutoa maelezo kwa ufasaha kwa Taasisi/ Afisa atakayepokea malalamiko, pia ni vema kwa mlalamikaji kutoa vielelezo vitakavyomsaidia Taasisi/ Afisa aliyepokea maelezo ili aweze kubaini aina ya malalamiko, sababu na kiini cha malalamiko na mamlaka inayowajibika kuyapatia ufumbuzi.

3.0 NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO:

Malalamiko yaliyowasilishwa ana kwa ana husikilizwa na afisa anayehusika na kushughulikiwa endapo malalamiko hayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Iwapo itabainika kuwa malalamiko yanapaswa kushughulikiwa na mamlaka nyingine tofauti na ofisi iliyopokea malalamiko hayo, mlalamikaji ataelekezwa kupeleka malalamiko yake kwenye mamlaka yanayohusika.

Malalamiko yaliyowasilishwa kwa njia ya maandishi ya wazi na yasiyo ya wazi yatasomwa kwa kina na afisa muhusika ili kuona kama yamekamilika na mlalamikaji atajulishwa kuwa yamepokelewa na kuanza kushughilikiwa ipasavyo na kwamba atajulishwa matokeo baada ya uamuzi kutolewa.

Baada ya uamuzi kutolewa kuhusiana na malalamiko yaliyowasilishwa, iwapo malalamiko yalikuwa yanaihusu taasisi au mamlaka au ofisi nyingine, ni vizuri kuiandikia taasisi au mamlaka au ofisi inayohusika kuijulisha uamuzi na kuitaka itoe taarifa ya utekelezaji wamaelekezo ndani ya siku 30 akielezea namna uamuzi au maelekezo yalivyoshughulikiwa.

Angalizo:

Inashauriwa kabla Mlalamikaji hajapeleka malalamiko dhidi ya Taasisi yote chini ya OR TAMISEMI  katika magazeti au luninga, ni vema awasilishe malalamiko yake kwa mdomo au maandishi katika Ofisi za Mitaa/Vijiji, Kata, Halmashauri, Mikoa na OR TAMISEMI kwa kutumia anuani au namba za simu zinazofahamika kwa urahisi wa kumaptia majibu dhidi ya malalamiko yake. Kwa ofisi ya OR TAMISEMI anuani imetolewa katika kipeperushi hiki.

4.0 HITIMISHO:

Katika maisha na hali ya kawaida si kila mtu anaweza kuridhika na kukubaliana na namna jambo linavyotekelezwa. Kadhalika sio kila mtekelezaji anaweza kutekeleza jambo vizuri, kwa usahihi na kwa kiwango cha kuridhisha na hii ndiyo sababu kubwa inayosababisha kuwepo kwa malalamiko katika jamii iliyotuzunguka.

Aidha, wateja ni miongoni mwa wadau muhimu katika kuhakikisha kuwa matatizo ya Watumishi wa wa Umma na wananchi wengine yanashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi kwa upesi ili kupunguza malalamiko. Wote tunao wajibu wa kushulighulikia malalamiko kwa wakati, kwa upesi na kwa usahihi na pia kufuatilia kwenye mamlaka husika ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa wakati kwa uamuzi na maelekezo zaidi kamaitabidi.

Kwa uelewa zaidi kipeperushi hiki kisomwe na Mkataba wa OR TAMISEMI wa Huduma kwa mteja. Malalamiko hayana budi kushughulikiwa kwa wakati na kwa ukamilifu kama sehemu ya kuunga mkono kauli mbiu ya Miaka 50 ya Uhuru inayosema:

Imetolewa na Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. 

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI

    May 18, 2025
  • WAUGUZI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

    May 12, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEIMOSI YAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

    May 01, 2025
  • MKURUGENZI AWATAKA WATUMISHI WOTE KUFANYA KAZI KWA UPENDO NA UADILIFU

    April 28, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.