Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija leo 5,Januari, 2026 amewashauri wananchi kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma wakati wote, amesisitiza kuwa Serikali imedhamilia kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wote ili wananchi waweze kuwa na uhakika wa matibabu.
Mheshimiwa Ludigija amewashauri wananchi kuwa tayari kujiunga na bima hiyo ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma za afya za uhakika ili kuepusha matatizo yanayojitokeza pindi ugonjwa unapojitokeza ghafla
" hii ni fulsa mtu akilipia hii bima atapata matibabu kama watumishi wanavyopata matibabu kwahiyo hii fulsa tuitumie vizuri ili tuweze kupata huduma za afya za uhakika"
Akitoa taarifa fupi ya kikao hicho mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Fredrick Mgarula amesema Serikali imeanzisha bima hii ili kuwahakikishia wananchi wote wanapata huduma za afya za uhakika mahali popote.
" lengo la kunzishwa bima ya afya kwa yote ni kuongeza uwajibikaji kwa Serikali na wananchi,kuleta usawa katika huduma, kwahiyo bima ni kuchangia fedha kwenye kapu moja ili mmojawetu akiugua fedha hiyo imsaidie kupata huduma kwa urahisi"amesema Mgarula
Katika kikao hicho wameshiriki wawakilishi wa makundi mbalimbali wakiwemo waendesha pikipiki,mama lishe,wafanya biashara,viongozi wa vyama vya wafanyakazi,viongozi wa dini,wazee maarufu na viongozi wengine ambao wameshauri elimu hii iendelee kutolewa kwa wananchi ili wengi wajue umuhimu wa bima ya afya kwa wote
Mheshimiwa Sabana Lushu Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kwimba ametumia kikao hicho kuwahamasisha wananchi wote kuona umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma bora za afya " ugonjwa unaweza kutokea ukiwa hauna hata fedha ya kwenda hospitali kwahiyo ukiwa na bima itasaidia kupata huduma bila kujali tuko kwenye mazingira gani, nimejifunza bima iliwahi kunisaidia nilipokosa msaada nikiwa natakiwa kufanyiwa upasuaji" amesema Sabana
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.