BALAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 4 YA MAPATO YA NDANI
Posted on: February 18th, 2025
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inatarajia kukusanya bilioni 4 kutoka mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2025/26.Wakijadili bajeti hiyo kwenye baraza la madiwani lililofanyika Feb. 17,2025 wamesisitiza miradi yote iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka huo itekelezwe .
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya,ndug Mohamed Ngasinda Katibu Tawala wa Wilaya amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuleta fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/25 pia ameipongeza Halmashauri kwa kusimamia utekelezaji miradi kwa weledi.
Aidha amewataka wasimamizi wa miradi kuendelea kusimamia miradi kwa weledi ili thamani ya fedha ionekane kwenye miradi hiyo
"Mipango yote mliyopanga mkaisimamie bila kuzembea, mwaka ujao 2025/26 mwende mkasimamie fedha hizi mlizobajetia lakini pia niendelee kuwasihi watendaji muendelee kusimamia miradi kwa kasi ileile mliyoonyesha mwaka huu unaoelekea kuisha" Ngasinda
Nao waheshimiwa madiwani wametaka miradi yote iliyopangwa itekelezwe ili kata zote ziwe na miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha taarifa ya mpango na bajeti wa mwaka wa fedha 2025/26 ndugu Rogatevane Kipigapas Afisa mipangi Wilaya amesema " katika mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri ilibajeti bilion 3.9 lakini katika mwaka ujao 2025/26 Halmashauri imepanga kukusanya bilioni 4 ambayo itaongezeka kutokana na ongezeko la vyanzo vipya vya mapato kama ufunguzi wa vituo vya afya,zahanati na shule ya mchepuo wa kiingereza.