Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa baraza la Madiwani limesisitiza elimu ya mpiga kura iendelee kutolewa kwa wananchi ili waweze kushiriki uchaguzi utakaofanyika Novemba 27,2024
" tuendelee kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi bora watakaoweza kuchochea maendeleo ya vijiji vyetu" amesema Mhe.Thereza Lusangija Mwenyekiti wa Halmashauri
Katika baraza hilo lililofanyika Novemba 13,2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri taarifa mbalimbali zimejadiliwa lakini msisitizo mkubwa ukiwa kwenye uhamasishaji na utoaji wa elimu ya mpiga kura
Naye Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe Shanif Mansour ameshauri vyama vyote vya siasa vishindane kwa hoja ili wananchi wamchague kiongozi kutokana na sera alizonazo
" Uchaguzi huu ni huru na haki kwahiyo twende tukafanye kampeni tuwashawishi wananchi wachague Viongozi wenye hoja za kuleta maendeleo tukashindane kwa sera kila chama kifanye kampeni ili wananchi wachague ni kiongozi yupi anayefaa" Shanif
Akiwasilisha taarifa ya maendeleo Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi Dkt Amon Mkoga amesema elimu ya mpiga kura inaendelea kutolewa kwa wananchi kupitia njia mbalimbali kama matamasha, bonanza, vyombo vya habari, machapisho na mikutano ya hadhara
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.