• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

BARAZA LA MADIWANI LAAZIMIA KUIGAWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KWIMBA ILI KUPATA HALMASHAURI NYINGINE MPYA

Posted on: February 19th, 2021


Kilio cha wakazi wa Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza cha kutaka mgawanyo wa Halmashauri mbili kinatarajia kutoweka, baada ya baraza la Madiwani la Halmashauri kuazimia kuigawa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, ili kupata Halmashauri mpya.

Wakizungumza katika kikao cha kuwasilisha mapendekezo ya ugawaji wa Halmashauri  tarehe 19/02/2021 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Madiwani wamesema wanayo shauku kubwa ya kupata Halmashauri mpya ili wananchi waweze kusogezewa huduma karibu na kuongeza chachu ya maendeleo.

Dhamira ya baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupitisha pendekezo hilo, ni kutaka kuongeza chachu ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Kwimba na kusogeza karibu huduma kwa wananchi.

" Sisi hitaji letu ni kupata idhini ya kuanzisha Halmashauri mpya  kwa vile vigezo tumetimiza tuombe hitaji letu lifanikiwe litakapofika ngazi za juu" amesema Peter Misalaba Diwani Kata ya Nyambiti.


Nae Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe.Kasalali Mageni amesema "Nawashukuru wote kuanzia Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi,Wakuu wa Idara na Madiwani kwa ushirikiano mnaoendelea kuuonyesha, ombi langu ushirikiano huu uendelee hadi tutimize hitaji letu la kupata Halmashauri mpya, tusikatishane tamaa,tusikwamishane njiani tushirikiane ili tutimize malengo ya kuwasogezea huduma wananchi ambalo ndiyo lengo la Raisi wetu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli"

Baada ya mapendekezo hayo kupitishwa, kikao hicho kinatarajia kuyawasilisha katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mwanza (RCC), ili kiweze kuweka baraka zake kisha  itapelekewa kwenye Wizara husika, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI) ili nao waweke baraka kama wataridhishwa na vigezo vilivyoorodheshwa  kwa ajili ya uanzishwaji wa Halmashauri mpya.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga amewapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa maamuzi hayo na amesisitiza kutokata tamaa pia ameshauri maandalizi ya kuongeza mapato ya ndani yaanze kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kiwango cha mapato kiongezeke zaidi.

 Katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba Bib.Pendo Malabeja ametoa taarifa na kuonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba  inavyo vigezo vinavyozingatiwa katika ugawaji wa Halmashauri ikiwemo kigezo cha mapato ya ndani kufikia bilioni mbili,idadi ya wananchi inakidhi,Taasisi za muhimu yaani Afya,Elimu na nyingine zipo.


Mapendekezo ya uanzishwaji wa Halmashauri mpya yamepitishwa na Madiwani wote wa kata thelathini za Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Madiwani kumi wa viti maalum walioridhia kuijenga Kwimba mpya.




Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.