Kampuni ya H.K imetoa pikipiki 12 kwa watendaji ili kusaidia katika shughuli za maendeleo ya kilimo cha zao la pamba
Akikabidhi pikipiki hizo Katibu Tawala ndugu Mohamed Ngasinda amewataka kwenda kusimamia zao hilo kwa umakini kwani Serikali inaendelea kuboresha zao la pamba ili kuongeza uzalishaji wa zao hii
" juhudi zilizopo ni kurudisha zao hili kwa kuboresha zao hili kupitia mbegu bora,mbolea na wataalamu wakusimamia maendeleo ya zao hili" amesema Ngasinda
Amewataka wataalamu hao walioaminiwa na bodi ya pamba na kupewa ajira hiyo kufanya kazi kwa bidii na kufanya kazi kama wataalamu ili kuongeza uzarishaji wa zao hilo.
Pia amewataka kwenda kutumia vizuri vitendea kazi vyote walivyopewa ikiwa ni pamoja na pikipiki " msibadirishe matumizi ya pikipiki hizi mkaanza biashara nyingine tunataka pikipiki hizi zikatumike kusimamia maendeleo ya zao la pamba, tunataka mkawe mnyororo wa kuonyesha maendeleo na kufikia lengo la uzarishaji wa pamba" amesema
Pia amewataka kwenda kuhamasisha wananchi kulima zao la pamba kwasababu Serikali inatoa mbegu kwa bei ya ruzuku na mbolea hivyo wakulima wengi wachague kulima zao hilo la pamba
Akiwasilisha taarifa mratibu wa mradi huo kutoka kampuni ya H.K amesema Wizara imewaruhu kufanya kazi japo kwa masharti ya kuwahudumia kwa kuwapatia usafiri maafisa ugani wote watakaofanya nao kazi ya pamba. Aidha kiwanda hicho kimefunguliwa ili kuanza kazi zake baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi.
Mtendaji wa Kijiji cha Mwalujo amewapongeza viongozi wa kampuni hiyo kwa kuamua kufufua kiwanda hicho ili kiweze kufanya kazi tena.
Nao maafisa ugani waliopewa pikipiki pamoja na vitendea kazi vingine wameishukuru kampuni na bodi ya pamba kwa ujumla kwa kuwawezesha kupata vitendea kazi vitakavyowarahisishia kazi ya usimamizi wa zao la pamba
Naye Martin Raphael Afisa ugani amesema " wengi tulikuwa hatuna ajira tumefurahi kupata ajira hii na tunaaahidi tutafanya kazi na kuleta matokeo chanya kwenye zao hili"

Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.