• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

DC-Kwimba Auomba Uongozi wa Wilaya Kutambua Wajibu Wake Katika Kutekeleza Mradi wa Mama na Mtoto

Posted on: January 24th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba  Mhandisi Mtemi Msafiri Simeoni ameuomba uongozi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kutambua wajibu wake katika kutekeleza Mradi wa Mama na Mtoto (MnM) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia taasisi za “International Development Research Center” (IDRC) na “Global Affairs Canada” (GAC) na kutekelezwa kwa ushirikiano na kamati ya Afya Mkoa  wa Mwanza na kamati ya Afya ya Wilaya ya Kwimba ili kusaidia vipaumbele vya Wilaya katika kuboresha afya ya mama na mtoto.

Mtemi aliyasema hayo wakati  akijitambulisha kwa wajumbe wa kikao cha kuutambulisha Mradi wa Mama na Mtoto kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo tarehe 23 Januari, 2018 katika ukumbi wa Ndilima Hoteli kata ya Hungumalwa Wilayani Kwimba.



Mkuu wa Wilaya ya Kwimba  Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon akijitambulisha kwa wajumbe wa kikao cha kuutambulisha Mradi wa Mama na Mtoto 


Akiongea katika kikao hicho Mratibu wa Mifumo ya Afya Bibi Magdalena Mwaikambo kutoka Mradi wa Mama na Mtoto alisema

“ Mradi  unawalenga akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano lengo likiwa ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupitia uboreshaji na utoaji wa huduma  muhimu za awali kwa mama mjamzito, wakina mama, watoto wachanga pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuboresha namna ya utoaji wa huduma za afya pamoja na utumiaji wa huduma muhimu  za makundi lengwa”.

Bibi Mwaikambo aliendelea kusema  wameamua kufanya kazi Kwimba kwa sababu takwimu zinaonesha kuwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano viko juu ukilinganisha na Halmashauri nyingine za Mkoa wa Mwanza.



Mratibu wa Mifumo ya Afya Bibi Magdalena Mwaikambo akielezea Malengo ya Mradi.


Kwa upande wake  Dr. Maendeleo Boniphance ( Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Bugando) chini ya Mradi wa Mama na Mtoto aliuomba uongozi wa Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha unasimamia zoezi kikamilifu ili kupata  wahudumu wa afya ngazi ya jamii watakaoweza kutekeleza majukumu yao  katika jamii na Mradi utatoa mafunzo ya huduma jumuishi ya Mama na Mtoto kwa watoa huduma kwa kufuata mtaala wa wizara ya afya.

Akiendelea kuchangia Dr. Maendeleo  alisema kuwa baada ya Mradi kukamilika tunatarajia  kuongezeka kwa idadi ya akinamama wajawazito wanaojifungua katika vituo vya afya,kuboreka kwa mawasiliano kati ya watoa huduma katika vituo na jamii inayohudumiwa, kuboreka kwa miundombinu ya vituo katika utoaji wa huduma za afya, vituo kuwa na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya huduma za afya ya  uzazi na mtoto pamoja na kuimarika kwa viashiria vya utoaji huduma.



 Dr. Maendeleo Boniphance ( Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Bugando) chini ya Mradi wa Mama na Mtoto akichangia Mada.

Kwa kuongezea  Mwezeshaji kutoka Mradi wa Mama na Mtoto Anthony Mlila  alisema Mradi utatoa  mafunzo rejea jinsi ya kumhudumia mama mwenye dalili za  kifafa/mwenye kifafa cha mimba, kutokwa damu nyingi baada ya kujifungu,kusaidia mtoto mchanga kupumua na kusambaza miongozo husika katika vituo vyote vya afya.

Aidha Afisa Mradi Ndg Leonard Masele  alichangia kwa kusema  Mradi huu utashirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya,Wakuu wa Idara na Vitengo,Kamati ya Afya ya Wilaya, Uongozi wa Kata,Kijiji,Kitongoji na jamii kwa ujumla.



 Afisa Mradi Ndg Leonard Masele  akielezea juu ya Ushirikishwaji wa Wadau mbalimbali katika kutekeleza Mradi

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A. Malabeja aliushukuru uongozi wa Mradi kwa kuleta mradi katika Halmashauri ya Kwimba na alisema uongozi wa Halmashauri ya Wilaya upo tayari kutekeleza Mradi  kwa umakini na weledi wa hali juu na wananchi wategemee kupata huduma bora za afya.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A. Malabeja akitoa shukrani zake kwa wawakirishi wa Mradi.

Mradi huu umechukuliwa kutokana na ufaulu uliojionyesha katika kutekeleza mradi kama huu nchini Uganda kupitia Health Child Uganda (HCU) ambao ulifadhiliwa na Global Affairs (GAC) katika mradi wa MUSKOKA ambao ulitekelezwa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbalala (MUST) mwak 2011 mpaka 2015 na kuonyesha matokeo chanya.

 

 

 

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.