DC LUDIGIJA AAPA KUWAFUNGA WANAOBAKA AU KUO WANAFUNZI
Posted on: July 12th, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka vijana na wanaume wote wanaoingia tamaa ya kuwashawishi na kuwabaka wanafunzi kuacha tabia hiyo mara moja kwani atakayebainika kumpa ujauzito au kuoa mwanafunzi atafungwa miaka 30 haijarishi mtuhumiwa atakuwa na umri gani
" tutawafunga miaka 30 bila kujali wewe ni mzee au kijana yaani ukibainika umebaka mwanafunzi maana tunachojua mwanafunzi ni mtoto kwahiyo hata kama alikubaliana na wewe sisi tunajua umembaka tutakufunga" Ludigija
Ameyasema hayo leo 12 Juni, 2025 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mantare na Sumve wakati akisiliza na kutatua kero za wananchi.
Mkuu huyo ametumia mkutano huo kuwahamasisha Wananchi kuzingatia maelekezo ya kiafya ili kujikinga na mlipuko wa magonjwa mbalimbali pia amewasisitiza wanawake wajawazito kuzingatia utaratibu wa kuhudhulia kliniki kwa wakati na kwenda kujifungua Hospitali.
Aidha amewataka viongozi wa Vijiji kutoa taarifa za waganga wa tiba asili wanaofanya ramli chonganishi ili wachukuliwe hatua
"Wenyeviti wa vijiji na vitongoji tuambieni kama kuna waganga wanafanya ramli za kuchonganisha watu ili tuwakamate, kama wewe ni mganga na umeona mtu ni mchawi pambana naye wewe siyo umwambie mtu eti umelogwa na fulani, tutawakamata" Ludigija
PiaWananchi wametakiwa kuzingatia malezi bora kwa watoto ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya mmomonyoka wa maadili
Wataalamu walioshiriki mkutano huo wametoa maelekezo mbalimbali kwa wananchi yakiwemo kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalumu wakike kwenye shule ya Msingi Kakora ambapo kituo kimeanzishwa cha kupokea watoto walema wenye umri wa kuanzia miaka mitano ili wakapate elimu na wataishi hapo shuleni bila kuchangia gharama yoyote.
Wananchi walioshiriki mikutano hiyo wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuona umuhimu wa kusikiliza kero na changamoto zao kwani maswali na changamoto zote zilizojitokeza zimepatiwa ufumbuzi.
Katika mikutano hiyo wananchi wamehamasishwa kushiriki uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, ambapo wameshauriwa kushiriki kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao.