Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija leo Oktoba 13,2024 amejiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Mkuu huyo ametumia wasaa huo kuwahamasisha Wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha waende kwenye vituo vilivyo maeneo wanayoishi ili wajiandikishe kwaajili ya kupata haki ya kupiga kura ya kuwachagua viongozi wa Serikali za mitaa.
Uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ulianza tarehe 11 Oktoba na utamalizika tarehe ishirini mwezi huu. Wananchi wote wameaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli hiyo ya Kitaifa.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya Kwimba na Sumve Dkt.Amon Mkoga amewahamasisha Wananchi waliokuwepo katika kituo hicho cha ngudulugulu kwenda kuwa mabalozi kwa familia zao na majirani zao kuwahamasisha kujiandikisha
" niwaombe mkawahamasishe wanafamilia wenu wote majirani zenu na ndugu wote waje wajiandikishe ili uchaguzi ukifika waweze kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka" amesema Mkoga
Wanachi waliokuwa wakijiandikisha katika kituo hicho wameahidi kwenda kuwahamasisha wananchi ambao bado hawajajiandikisha ili nao wajiandikishe " niwashauri wengine waje wajiandikishe ili siku ya Uchaguzi tumchague Mwenyekiti tunayemtaka" amesema Getruda Malisu
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.