DC LUDIGIJA AHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA SIKU YA UCHAGUZI MKUU 2025
Posted on: October 2nd, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija amewahamasisha Wananchi kujitokeza siku ya uchaguzi kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi watakaohamasisha maendeleo.
"Kilichotukutanisha hapa leo nikukumbushana kuwa tarehe 29,Oktoba 2025 itakuwa siku ya uchaguzi hivyo wananchi wote ni haki yenu kwenda kupiga kura kwenye vituo mlivyojiandikisha"amesema Ludigija
Pia amwataka wananchi kulinda amani ya Taifa kwa kutojihusisha na shughuli zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani siku hiyo "Niwaombe sana tujiepushe siku hiyo na mambo yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani, twende kupiga kura na turudi nyumbani tusubiri matokeo"Ludigija
Pia amewakumbusha kuwa kiongozi atakayepatikana atatokana na kura zilizopigwa hivyo kila Mwananchi anatakiwa kupiga kura ili kumpata kiongozi anayemtaka
"Ile kasumba ya kusema sipigi kura maana kiongozi ameshapita achaneni nayo maana kila mtu akisema hivyo hatutapata kiongozi tunayemtaka hivyo kupiga kura ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.
Pia amewataka kwenda kuwa mabalozi kwa watu wengine kuwakumbusha kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 wote kwenda kupiga kura.
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba ametumia wasaa huo kuwahamasisha Wananchi wote kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura ili kuwapata viongozi watakaoleta maendeleo.
Aidha msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwimba na Sumve ametumia wasaa huo kuwaelekeza na kuwakumbusha wananchi taratibu zitakazotumika siku ya uchaguzi kwenye kituo cha kupigia kura, huku akiwasisitiza kuwa atakaye ruhusiwa kupiga kura ni yule aliyejiandikisha kwenye daftari la mpiga kura na atatakiwa kufika kwenye kituo cha kupigia kura akiwa na kitambulisho chake.
Wananchi waliofika katika tamasha hilo wameonyesha kuwa wanayo shauku ya kufika siku ya uchaguzi ili wakatumie haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka.