DC LUDIGIJA AISHUKURU TAASISI YA DORIS MOLEL KWA KUJENGA JENGO LA WATOTO NJITI
Posted on: August 5th, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija ameishukuru Taasisi ya Doris Molel Foundation kwa kuona umuhimu wa kujenga jengo la watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba
Akiongea na mfadhili wa shirika hilo Bwana Antonio Luic Antonio ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la KCA ( Keep a Child alive) amewashukuru kwa kutoa zaidi ya bilioni 1.5 kwaajili ya kufanikisha mradi ambapo bilioni 1.4 kwaajili ya jengo la watoto njiti, vitanda na vifaa tiba na fedha nyingine ni kwaajili ya ujenzi wa nyumba mbili za watumishi ambapo kila nyumba itajengwa kwa milioni 92.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Dr. Fredrick Mgarula amesema kukamilika kwa majengo hayo kutasaidia upatikanaji wa huduma bora kwa watoto njiti, pia itapunguza au kuondoa kabisa vifo vya watoto njiti kwani huduma bora zitapatikana Wilayani hapa hakutakuwa na haja ya kupeleka watoto hospita ya Mkoa ambayo iko mbali zaidi ya kilomita 90 kutoka Kwimba.
Aidha Mganga Mkuu akiwasilisha taarifa hiyo amewaomba wafadhili hao kama itawezekana kuongeza nyumba nyingine za watumishi ili kusaidia watumishi kuishi karibu na hospitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za dharura.
Naye Doris Molel amewaeleza Wafadhili hao kuwa ujenzi unaendelea vizuri na mahitaji ya majengo hayo ni makubwa sana kwani watoto njiti ni wengi na wanahitaji huduma bora.
Bwana Antonio ametembelea wodi ya watoto njiti inayotumika kwa sasa ambapo ametoa zawadi kwa wazazi wa watoto hao kisha amekagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambapo amepongeza kwa hatua iliyopo pia amesema anao wito wa kusaidia watoto njiti ili waishi ndio sababu alianzisha Shirika linaloitwa " Keep a Child alive "