Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija amekabidhi pikipiki tatu kwa maafisa afya wa kata kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya ngazi ya jamii, hususani katika maeneo ya vijijini.
Akikabidhi pikipiki hizo amewataka maafisa afya kuzitumia kwa uangalifu na kwa kuzingatia taratibu za matumizi ya mali za umma ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Wilaya ya Kwimba
“ pikipiki hizi zitasaidia kuimarisha ufuatiliaji wa huduma za afya ya msingi, utoaji wa elimu ya afya kwa jamii, pamoja na ufuatiliaji wa wagonjwa katika maeneo yao ya kazi, hasa katika maeneo yenye changamoto za miundombinu ya usafiri.”amesema Ludigija
Kwa upande wao, maafisa afya waliokabidhiwa pikipiki hizo wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha vitendea kazi hivyo, kuwa sehemu ya msaada katika kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi na kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.