• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

DC LUDIGIJA AMEITAKA KWIMBA KUENDELEA KIUCHUMI KUPITIA KILIMO

Posted on: February 3rd, 2023


Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ngw’ilabuzu Ndatwa Ludigija Leo Februari 3,2023 akiripoti Wilayani Kwimba amemkuta Balozi wa Pamba Mheshimiwa Agrey Mwanri akitoa semina za umwagiliaji wa viuwadudu vya Pamba hapo akatoa neno Kwa washiriki wa mafunzo hayo ambao walikuwa ni watendaji wa Kata na vijiji , wakulima wa mfano, maafisa ugani, viongozi wa AMCOS na wataalamu kutoka Halmashauri.


“ Mimi ni mkulima mzuri sana na hapa Kwimba ni nyumbani kwahiyo niwaombe wanakwimba tulime kilimo  cha kisasa chenye tija tena siyo kilimo cha mazao ya chakula tu!, tulime na mazao ya biashara angalau zao moja la biashara hasa Pamba  Ili kupitia zao hilo tuinuke kiuchumi tuendelee zaidi ya hapa tulipo” amesema Ludigija


Aidha Mkuu wa Wilaya amesema anawataka washiriki wa mafunzo hayo  kuwa mabalozi kama Agrei Mwanri Ili Kila mwananchi ahamasike kulima kilimo bora tena kilimo kitakachoifanya kwimba inabadirika, vilevile amewataka wananchi kutoa ushirikiano Ili kufanikisha malengo ya kuiendeleza Kwimba.


“ hiki ni kipindi cha kumwagilia dawa za kuuwa wadudu, tukifanikiwa hapa tutakwenda mbele zaidi maana tunataka zao la Pamba  liwe ndio zao la biashara namba moja hapa Kwimba Ili hata viwanda vilivyokuwa vinaanza kupotea vianze kazi tena” Ludigija


Katika semina hiyo Balozi wa Pamba Mheshimiwa Agrey Mwanri amewataka viongozi na wataalamu walioshiriki semina hiyo kwenda kufikisha elimu ya umwagiliaji wa viuwadudu Kwa wananchi Ili kusaidia kupambana na wadudu wanaoshambulia Pamba.


“ nendeni mkawe mabalozi tunataka kupambana na hawa wadudu wanaoshambulia Pamba, vilevile  wafikishieni taarifa wananchi kuwa mwezi wa Saba tutapita kukagua kama maotea yote ya Pamba yameng’olewa, watakaokutwa bado hawajayatoa Sheria zitachukuliwa dhidi yao” Mwanri


Mheshimiwa Mwanri atafanya ziara ya siku tatu hapa Kwimba ambapo anatarajia kupita  vijijini  kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba hasa namna  bora ya umwagiliaji wa viuwadudu vinavyoonekana kuwa tishio Kwa zao la Pamba.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.