DC LUDIGIJA ARUDI SHIGANGAMA KUTOA MREJESHO WA KERO ZA KIJIJI HICHOO
Posted on: July 24th, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija ametoa mrejesho wa utatuzi wa kero za kijiji cha Shigangama baada ya kero hizo kuwasilishwa kwenye mkutuno wa kusikiliza na kutatua kero uliofanyika miezi michache iliyopita.
" mnakumbuka awamu iliyipita nilifika hapa mkaeleza kero ya upatikanaji wa maji hakuna mabomba wala visima,barabara mbovu na uchakavu wa miundombinu ya Shule ya msingi hasa vyoo havikuwepo, sasa mumeona utekelezaji umefanyika madarasa yamejengwa,vyoo vimejengwa pia gari la kuchimba kisima lilikuja hapa lakini walipochimba hawakukuta maji kwahiyo maji tunasubiri mradi wa maji ya ziwa Victoria kwasababu upande wa visima imeshindikana" amesema Ludigija
Pia ameutumia mkutano huo kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi na muwekezaji anayetaka kuanzisha shughuli za kilimo, ambapo amewaelekeza wataalamu wa arshi na watu wengine kufika eneo hilo ili kukutana na wananchi wanaoishi katika eneo hilo pamoja na mmiliki ili wakague na kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwang'hanga amewashauri wananchi wenye mgogoro huo wa ardhi wakubali kutatua mgogoro huo kwa amani kati yao na muwekezaji ili wasifukuzwe eneo hilo maana kama wataondolewa itakuwa usumbufu kwa wanafunzi
Katika mkutano huo ameshiriki Katibu CCM kata ya Shilembo ambaye ameshauri Mgogoro huo utatuliwe kwa umakini zaidi ili wananchi wasihamishwe wakapata usumbufu.
Eneo hilo lina hati ya mwaka 1987 hivyo wananchi wanaoishi wameshauliwa kutoa ushirikiano kutatua mgogoro huo kati yao na mmiliki wa eneo hilo ili mmiliki wa eneo hilo apate haki na wananchi wanaoishi eneo hilo wapate haki
Wananchi wamemuomba Mkuu wa Wilaya kusimamia utatuzi wa mgogoro huo ili kila anayeguswa na mgogoro huo apate haki yake