Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wameendelea kupita mtaa kwa mtaa wakihamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Mkuu huyo ametumia wasaa huo kuwaelewesha Wananchi kuwa uandikishaji wa sasa ni tofauti ule uandikishaji ambao wananchi wanapewa kitambulisho
" wananchi mnatakiwa mjue kuwa ule uandikishaji mliopewa kitambulisho ni kwaajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2025 wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani lakini huu uandikishaji wa sasa hivi kwanza haupewi kitambulisho ni kujiorodhesha kwenye daftari ili siku ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uweze kumchagua Mwenyekiti wa Kijiji chako na kitongoji pamoja na wajumbe wa Serikali ya kijiji" Ludigija
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wameendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari ambapo kufikia jana zaidi ya asilimia 80 ya lengo la Wilaya walikuwa wamejiandikisha.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.