• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

DC LUDIGIJA AZINDUA ZAHANATI YA NYAMATALA NA KUFUNGUA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA ISUNGA

Posted on: May 8th, 2023


Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija Leo Mei 8,2023 amezindua Zahanati ya Nyamatala iliyopo Kata ya Ngula.Akizindua Zahanati hiyo Mheshimiwa Ludigija amewataka Wananchi kuitumia Zahanati hiyo kupata huduma za Afya hasa wanawake wajawazito na watoto Ili kuepuka vifo vinavyoweza kuzuilika.


" wito wangu kwenu acheni tabia ya kupeleka wagonjwa kwa waganga wa jadi, yaani mtu akiugua kituo cha kwanza iwe kwenye Zahanati, tena waganga wa jadi muwe mabalozi akija kwenu mgojwa mshauri aende Hospitali kwanza, kwamfano wajawazito mnawapa dawa zinazosababisha madhara makubwa kwa watoto acheni hiyo tabia na atakayebainika anapokea wajawazito tutamchukulia hatua" Ludigija


Mkuu huyo ameitumia hadhara hiyo kuwaeleza Wananchi kupeleka watoto wao shuleni Ili kutokomeza ujinga na kuongeza wasomi

" hakikisheni mnasomesha watoto wenu, angalieni hawa vijana waliopangiwa kazi hapa Nyamatala wamesomeshwa na wazazi wao nanyie mtamani kuona watoto wenu wakiwa Madakitari,Walimu, wahandisi  na wataalam wengine somesheni watoto" Ludigija


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo na amewashauri kulitumia ipasavyo kwa kuhakikisha wanapata huduma za Afya pia amewashauri kuitunza miundombinu ya Zahanati hiyo Ili idumu.


Wananchi wa Kijiji hicho wameishukuru Serikali kwa kuleta fedha millioni 50 kwaajili ya kukamilisha Zahanati hiyo "Kabla hatujapata hii Zahanati tulikuwa tunateseka kufuata huduma mbali na Kijiji na hiyo ilipelekea wanawake wengi kujifungulia nyumbani hivyo kusababisha wengine kufariki kwahiyo tunaishukuru Serikali kutukamilishia Zahanati hii" amesema  Judith Elias


Zahanati ya Nyamatala ilianzishwa kwa nguvu za Wananchi  na baadhi ya wafadhili wakiwemo kanisa la Baptist ambao walichangia zaidi ya millioni 50.


Aidha Mkuu wa Wilaya amefungua huduma za Afya katika Kituo cha Afya Isunga ambapo walipokea millioni 500 kwaajili ya ujenzi huo na jengo la wagonjwa wa nje,kichomea taka  na Maabara vimekamilika na majengo ya wazazi na jengo la kufulia yamefikia hatua ya ukamilishaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.