• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

DC LUDIGIJA AZITAKA TAASISI NA HALMASHAURI KUHAKIKISHA FEDHA ZA MIRADI ZINATEKELEZA MIRADI

Posted on: February 12th, 2025



Mkuu wa Wilaya ya Kwimba  Mhe Ng'wilabuzu Ludigija  amewataka viongozi wa Taasisi na Halmashauri  kuhakikisha fedha zinazopokelewa kwaajili ya kutekeleza miradi zitumike kwa wakati na miradi ikamilike na kutoa huduma

" tunataka tuone fedha zilizoandikwa kwenye hizo karatasi mnazosoma zionekane kwa uhalisia kwenye miradi husika hatutaki maneno" amesema Ludigija

Haya yamejiri kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya kilichofanyika leo Februari 12,2025 kikiwa na lengo la kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26.

Mheshimiwa Ludigija  ametumia kikao hicho kuwataka maafisa maendeleo wa Kata kuvisaidia vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kuandaa maandiko na katiba za vikundi ili iwe rahisi kuomba mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri.

Pia amewataka watendaji wa Kata kuwakamata watu wote wanaokwamisha shughuli za elimu ikiwa ni pamoja na wazazi ambao watoto wao ni wanafunzi lakini bado hawajaripoti shuleni hasa wale wanaoanza kidato cha kwanza

"Kamateni watu wote ambao watoto wao bado hawajaripoti shuleni wawambie hao wanafunzi wako wapi na kama kuna viongozi wanaowakwamisha huko ngazi za vijiji nao wakamateni wakiwasumbua nipeni taarifa" amesema Ludigija

Katika kikao hicho bajeti za taasisi zilizopo Wilayani hapa zimejadiliwa zikionyesha vipaumbele vya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha taarifa ya Halmashauri Ndugu Yohana Muhandikila kwa niaba ya Mkurugenzi  amesema kuwa katika mwaka 2025/26 Halmashauri  imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu,afya  na miradi ya utawala.

Naye Makam Mkuu wa Chuo cha Michezo Malya ndugu Denis Kayombo  ametumia kikao hicho kuwakaribisha wanakwimba na wananchi wote kupeleka vijana kusoma katika chuo hicho bora kabisa na cha pekee Afrika Mashariki

" Chuo ni chetu kipo Wilayani kwetu na sasa hivi kuna mradi mkubwa wa bilioni 32 unaendelea ambapo inajengwa Akademi ya michezo ( sports  academy) lakini wanakwimba hawapo, niwasihi muwalete vijana wasome michezo, siku hizi watu wanatajirika kupitia michezo " amesema Denis Kayombo

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.