Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt. Amon Mkoga amewataka wasimamimizi wa miradi ngazi ya Kata kuhakikisha wanaongeza kasi ya utekelezaji ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo Oktoba 9,2025 wakati akifanya ziara ya Kata kwa Kata kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi na shughuli nyingine
" nawapa wiki moja kukamilisha miundombinu yote, baada ya wiki moja nitarudi hapa Kikubiji kukagua hiki kituo cha Afya " alisema Mkoga
Aidha amewataka wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa madarasa Kata ya Mhande na Walla kuongeza juhudi zaidi ili kukamilisha miradi kwa wakati
Pia ametumia ziara hiyo kuongea na watumishi Kata ya Kikubiji,Nyamilama,Mhande na Bupamwa ambapo amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kutimiza wajibu wao.
Mkoga ametumia ziara hiyo kukagua vyanzo vya mapato ambapo wanaosimamia ukusanyaji wa mapato wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa uaminifu.


Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.