Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wakuu wa taasisi zote zilizopo Wilayani Kwimba kuhakikisha wanassimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha zote za miradi zinatekeleza miradi kwa wakati kabla ya mwaka wa fedha kuisha
" siyo vizuri fedha zinakuja kutoka Serikali kuu harafu zinakaa muda mrefu bila kutekeleza miradi iliyokusudiwa, kwahiyo fedha za miradi ya maendeleo nitazifuatilia kwa karibu sana" amesema Ludigija
Mkuu wa Wilaya ameyasema haya kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya kilichofanyika leo Desemba 18,2024 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo taarifa za taasisi za RUWASA,TARURA,Halmashauri na taarifa nyingine zimewasilishwa kwenye kikao hicho.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameitaka taasisi ya RUWASA kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Shighumlo- Nyamilama ili akamilishe mradi huo huku akisisitiza mtandao wa mradi huo ukamilike haraka ili wananchi wapate huduma pamoja na shule ya sekondari Nyamilama ipate maji ya uhakika
" tunatarajia kuanzisha kidato cha tano na sita hapo shule ya Nyamilama kwahiyo maji yanatakiwa yapatikane ya uhakika ili wanafunza wapate maji ya kutosha" Ludigija
Mheshimiwa Ludigija ametumia kikao hicho kutoa maelekezo kwa watumishi wote wa Idara ta Afya kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasanyo, pia amewataka watumishi wote wasiotimiza wajibu wao wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa watumishi wengine.
Katika kikao hicho ameshiriki Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Thereza Lusangija ambaye amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza utumishi wa umma.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt.Amon Mkoga ametumia wasaa huo kuwasisitiza watumishi wa idara ya afya kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.