• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

HALMASHAURI YAPONGEZWA KWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI NA UKUSANYAJI MAPATO

Posted on: May 29th, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija ameipongeza Halmashauri kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi hali iliyopelekea Halmashauri kununua gari ( Lori) lililopokelewa leo, ameyasema hayo leo Mei 29,2024 kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya tatu 2023/24.


" niwapongeze kwa kazi kubwa mnayofanya hadi kufanikisha mapato ya ndani kutekeleza miradi mikubwa, haya mambo tulizoea kuyaona kwenye Halmashauri za manispaa na majiji lakini Kwimba mnayaweza hongereni sana" Ludigija


Nao Waheshimiwa Madiwani wameipongeza Halmashauri chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato hali iliyopelekea Halmashauri kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, ukmilishaji wa Maabara,bweni,ununuzi wa gari (lori), ujenzi wa jengo la kusubilia wagonjwa Hospitali ya Wilaya,ujenzi wa vibanda soko la Ngudu mjini na shughuli nyingine.


" niwapongeze wataalamu kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato hili jambo liendelee maana Halmashauri yeti inategemea mapato ya ndani yanayotokana na ushuru wa mazao hivyo tuendelee kusimmia ili mapato yaongezeke lakini wanaokata ushuru wawazingatie wakulima wanaotoka kuvuna"  amesema Mayala Sagini Diwani Mwandu


Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya robo mwaka ya Halmashauri Bi. Happiness Msanga Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri amesema katika robo ya tatu Halmashauri imepokea fedha za kutekeleza miradi mbalimbali pia imepokea  magari ya wagonjwa ( ambulance) tatu, pia Halmashauri imenunua gari aina ya lori kwaajili ya kusaidia kazi mbalimbali za Halmashauri.


Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba Ndugu Aziza Isimbula ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi " niwapongeze kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kutekeleza miradi mbalimbali inayoonyesha wazi kuwa mnatekeleza ilani  ya CCM"


Katika Mkutano huo ameshiriki Mbunge wa Jimbo la Sumve Mheshimiwa Kasalali Mageni ambaye ameipongeza Halmashauri kwa kujenga kituo cha Afya Budushi Jimbo la Sumve  kwa fedha za mapato ya ndani.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.