• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Halmashauri Zaagizwa Kusomesha Walimu wa Michezo

Posted on: December 21st, 2017

Halmashauri za Mkoa wa Mwanza zimeagizwa kusomesha walimu wa michezo wawili kwa kila Halmashauri kwa gharama ya Shilingi 1,040,000/= kwa kila mwalimu  katika Chuo cha Michezo  Malya kilichopo katika Mkoa wa Mwanza Wilayani Kwimba ili kukuza vipaji vya michezo kwa wanafunzi.

Maagizo hayo yalitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Mwanza Mhe Elisha Hilary wakati wa   kikao cha ALAT  kilichofanyika Wilayani Kwimba tarehe 21 Disemba, 2017.

Akiongea chuoni hapo Mkuu wa chuo cha Michezo Malya Ndg Richard Timothy Maganga alisema nia na madhumuni ya chuo ni kutengeneza wataalamu wa michezo ili kutoa mafuzo na kuwa na usimamizi sahihi wa michezo katika maeneo yote nchini, ili kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo nchini.




Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya  Michezo Malya Ndg Richard Timothy Maganga akitoa Taarifa ya Chuo  kwa Wajumbe wa ALAT  Tawi la Mkoa wa Mwanza.

Akiendelea kuchangia mada Mwenyekiti wa ALAT Mkoa Mhe. Hilary aliipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba   kwa kulima zao la pamba kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kulima pamba kama zao kuu la biashara.

"Tunatarajia kupata kilo 40,800 kwa shamba  lote la ekari 68 sawa na wastani wa kilo 600 kwa ekari ingawa tulikumbwa na changamoto kipindi cha upandaji baadhi ya eneo la shamba lilituwamisha maji na kusababisha mbegu kuoza.Pia katika kilimo hifadhi baadhi ya magugu sugu hayakudhibitiwa vizuri na hivyo kuongeza gharama za palizi".

Hayo yalisemwa na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kwimba Bi Magreth Kavalo wakati akisoma taarifa  ya shamba la pamba la kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na  Wakuu wa Idara na Vitengo kwa wajumbe wa ALAT Mkoa wa Mwanza walipotembea shamba la mfano  la  watumishi Kilyaboya.



Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kwimba Bi Magreth Kavalo akisoma Taarifa  ya Kilimo kwa Wajumbe wa ALAT  Tawi la Mkoa wa Mwanza wakati wa Ziara ya kutembelea  Shamba la Mfano la Watumishi Kilyaboya.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Ndg John Wanga aliwaomba Wajumbe wa ALAT kuwa kikao kijacho kitakachofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kijadili mambo ya kubadilishana uzoefu katika ufanisi wa kazi mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri ikiwemo shughuli za miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Ndg John Wanga akichangi Mada wakati wa Mkutano Mkuu wa ALAT.

Mkutano Mkuu wa ALAT Tawi la Mkoa wa Mwanza Ulifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ukifuatiwa na Ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.