"hata huku mapolini tunaweza kupata Mawaziri,Raisi,Walimu,Madaktari na viongozi wengine"kauli hii imesema na Ndugu John Mihayo Cheyo Mkurugenzi wa mipango na sera kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Mihayo Cheyo iliyoko Kijiji cha Kiliwi Kata ya Bupamwa Wilayani Kwimba.
Cheyo ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wazazi kusomesha watoto wao na kuhakikisha kila mtoto anafikia ndoto yake huku akisisitiza kuwa kama shule imejengwa maeneo hayo basi wanafunzi wahimizwe kusoma ili wapatikane viongozi wa baadaye.
Shule ya Sekondari Mihaya Cheyo ilianza mwala 2023 ambapo wanafunzi waliokuwa wanasoma katika Shule ya Sekondari Bupamwa walihamishiwa shuleni hapa ili kuwapunguzia umbali mrefu waliokuwa wanatembea kutoka vijiji vya Kiliwi na Itegamatu ambapo walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita 19 kwenda shule ya Bupamwa.
Akihutubia mahafali hiyo Mgeni rasmi Ndugu John Mihayo ambaye shule hii ilipewa jina lake amewaasa " namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu kuleta fedha huku polini ili zijenge shule hii, pia amewashukuru na kuwapongeza wazazi wa wanafunzi ambao waliruhusu wanafunzi hao kusoma"
Naye Katibu Tarafa ya Mwamashimba amewataka wazazi kuweka kipaumbele kuwasimamia watoto wao kwenda shule ili kuondokana na changamoto ya utoro ambayo inaonekana kuwa tatizo kutokana na kukosekama muamko wa elimu.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Rogatevane Kipigapas amewasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kujiandaa na mitihani ya Taifa ili wapate ufaulu mkubwa utakaokuwa kumbukumbu nzuri katika shule hiyo kwani wanafunzi hao ndio wahitimu wa kwanza.
Akisoma taarifa ya Shule hiyo Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Frank amesema Shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa walimu kwani shule ina Walimu tisa tu wakiume saba na wakike wawili, pia amesisitiza kuwa pamoja na kuwa na walimu wachache wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafunzi wao ambao ni wahitimu wa kwanza wanafaulu.


Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.