Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt Amon Mkoga amepokea vishikwambi kutoka Shirika la ICAP( International Centre for AIDS care and treatment Program) kwaajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma ya mkoba ya kusajili wateja kwenye jamii.
Akikabidhi vishikwambi hivyo Mariam Masoud Afisa takwimu wa shirika hilo ameshauri vifaa hivyo kutumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa ili huduma iweze kuwafikia wateja katika maeneo yao
" wateja wengi walikuwa wanapata shida ya kutembea umbali mrefu kwenda kusajiliwa kwaajili ya kupata huduma za Afya sasa tumeleta vishikwambi hivi ili huduma zipatikane kwa urahisi katika vijiji" Mariam
Dkt. Amon akipokea vifaa hivyo amelishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kurahisisha upatikanaji wa huduma hasa usajili wa WAVIU ( watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi) na ameahidi kusimamia vifaa hivyo kufanya kazi iliyokusud
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.