Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt Amon Mkoga akiwataka watumishi wote kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa weledi
" kafanyeni kazi, watumishi wote timizeni wajibu wenu nataka kuona kila mtu katika eneo lake anafanya kazi zote,Ukiona kazi zako hazitekelezwi mpaka nikusimamie basi ujue hunifai" amesema Mkoga
Haya yamejiri kwenye kikao cha Mkurugenzi na watumishi wa makao makuu ya Halmashauri kilichofanyika leo Februari 14,2025 katika ukumbi wa Halmashauri.
Katika kikao hicho amewataka watumishi wa Idara ya manunuzi,Elimu Msingi na Sekondari kuongeza juhudi katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za Idara hizo, pia amewataka maafisa elimu kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa kuongeza usimamizi na motisha kwa walimu wanaofanya vizuri
Aidha Mkoga ametumia kikao hicho kumpongeza Mganga mkuu wa Wilaya kwa kuendelea kusimamia na kuboresha utoaji wa huduma za afya, pia amemtaka kuendelea boresha zaidi huduma hizo ili wagonjwa wapate huduma nzuri na kauli nzuri zitumike wakati wa kuhudumia wagonjwa.
Watumishi walioshiriki kikao hicho wameahidi kuendelea kutekeleza kazi zao kwa weledi na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi.