Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi ndugu William Kasuja leo tarehe 27 Novemba 2025 amewataka wajumbe wote kuzingatia mafunzo hayo ili kwenda kuandaa bajeti kwa kuzingatia dhima na malengo ya Halmashauri.
Pia amewataka kuzingatia vifungu vyote muhimu ili kuhakikisha shughuli zote zinatekelezwa kama ilivyokusudiwa.
Pia amewataka maafisa mipango kuhakikisha elimu hii ya kuandaa bajeti inatolewa kwa wataalamu ngazi ya Kata na vijiji ili waweze kuandaa bajeti zao kwa ufasaha.
Naye katibu wa mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango Paul Lubili amesema mafunzo hayo yanalengo kuongeza uelewa kuhusu uandaaji wa mpango na bajeti katika mamlaka ya Serikali za mitaa.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema "Tunawashukuru wawezeshaji, tumejifunza na tumeelewa hivyo tunaamini tutaandaa bajeti kulingana na maelekezo tuliyopewa pia tutakapohitaji msaada zaidi wa maelekezo muwe tayari kutuelekeza"amesema Afisa utumishi Khadija Mkelenga kwa niaba ya washiriki wa mafunzo.

Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.