• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO SHINYANGA

Posted on: April 13th, 2022

Kamati ya fedha, Uongozi na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba  yafanya ziara ya mafunzo  katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kujifunza  namna shughuli mbalimba za ukusanyaji wa mapato katika migodi wa Wilaya hiyo inavyotekelezwà


Ziara hiyo ilifanyika kuanzia  tarehe 12-13 ,Aprili 2022  katika mgodi wa Nyandolwa  ilikua na lengo la kujifunza mbinu mbalimbali ambazo wataalam wa Halmashauri hiyo wanazitumia ili kukusanya mapato katika migodi ya Wilaya hiyo.


Wajumbe wa kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Theleza Lusangija na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga, Waheshimiwa Madiwani na Wataalam walipata nafasi ya kujifunza utaratibu mzima wa shughuli zote zinazofanyika migodini ikiwemo uchimbaji wa madini,uchenjuaji na uuzaji wa dhàhabu na jinsi shughuli hizo  zinavyosaidia katika kuinua uchumi wa Wilaya hiyo.


Katika Mgodi wa Nyandolwa Kamati iliweza kukutana na Mwenyekiti wa kamati ya ukusanyaji wa mapato katika mgodi huo Ndugu Ephafras Mazina ambaye aliweza kuelezea jinsi kazi za mgodi huo zinavyofanyika na jinsi wanavyoweza kudhibiti utoroshaji wa dhahabu na hivyo kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo


"Katika mgodi huu tunayo timu inayosimamia ukusanyaji wa mapato, tunahakikisha kila mfuko wa mawe unalipiwa ushuru, wanaojishughulisha na biashara zote wanalipa ushuru, wenye magari ya kubeba mizigo na vyombo vingine vya usafiri wanalipa ushuru kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na wanaokiuka utaratibu wanatozwa faini kwa mujibu wa sheria" alisema Mazina


Aidha kamati hiyo iliweza kutembelea maeneo mengine ikiwemo eneo inapojengwa hospitali ya Wilaya hiyo na kuona shughuli hiyo inavyotekelezwa, katika eneo hilo Mhandisi amabaye alielezea mbinu wanazotumia ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa.


Wajumbe wa kamati hiyo waliweza kuzungumza na Kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndugu Stewart Makali  ambaye aliwakaribisha katika Wilaya hiyo na akawaeleza kwa kifupi Shughuli za kibiashara zinazofanyika katika Wilaya hiyo, kisha wajumbe waliahidi kwenda kufanyia kazi yale mazuri yote waliyojifunza kutokana na ziara hiyo.


Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.