• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: October 29th, 2022


Katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufasaha, leo tarehe 29, Oktoba 2022 kamati ya fedha uongozi na mipango imefanya ziara  katika maeneo mbalimbali kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Kamati hiyo imekagua kikundi cha Wanawake Wakulima Isagala ambacho kikundi  kilikopeshwa milioni 60 na Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba( mkopo usio na riba)  ambapo kupitia fedha hiyo kikundi kimenunua trekta linalotumika kulima na kusafirisha mizigo, trekta hiyo imenunuliwa mwezi  Septemba na kuanza kazi mwezi Oktoba. Tangu chombo hicho kianze kazi kimesaidia kuwaongezea kipato ambapo hadi kufikia leo kikundi kimekusanya milioni 4. Pia kikundi hicho kinajishughulisha na ufugaji wa ng'ombe  ambapo kwa sasa wana ng'ombe 25.


" trekta hii inatumika kukodi kwa watu wanaohija kulima mashamba ambapo heka moja tunalima kwa shilingi 45,000 kwa hiyo inatusaidia maana ndani ya mwezi mmoja tumepata milioni nne japo mvua ingekuwa imeshaanza kunyesha tungepata fedha nyingi zaidi maana kazi zingekuwa nyingi" amesema Yasinta Heneriko katibu wa kikundi


Aidha kamati imekagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati Kilyaboya, mradi unaotekelezwa kwa milioni 152 fedha za mpango wa kunusuru kaya maskini. Hapo kamati imeshauri kasi ya utekelezaji wa mradi iongezwe ili mradi ukamilike kwa wakati.


Kamati haikuishia hapo imefika Shule ya Sekondari Nyamilama ambapo wamekagua ujenzi wa madarasa 12 kwa milioni 240 fedha kutoka Serikali kuu ambapo madarasa haya ni miongoni mwa madarasa 112  yanayotekelezwa kwa bilioni 2.4 fedha kutoka Serikali kuu. Katika mradi huu majengo yako hatua ya msingi na kamati imeshauri kasi ya utekelezaji wa miradi hii iongezwe ili miradi ikamilike kwa wakati.


Ikikamilisha ziara hiyo  kamati imekagua ukamirishaji wa maabara katika Shule ya Sekondari igongwa ambapo milioni 30 ilipokelewa kwaajili ya kukamilisha maabara, maabara hiyo imekamilika na kuwekewa vifaa vyote vinavyotakiwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.