• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Kamati ya Lishe ya Wilaya Yaombwa Kuhamasisha Masuala ya Lishe

Posted on: August 29th, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kwimba Bibi Pendo A.Malabeja ameiomba kamati ya lishe ya Halmashauri ya Wilaya Kwimba kuhamasisha  masuala ya Lishe kwa watoto,wasichana,wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.

Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Uhamasishaji kuhusu maswala ya Lishe kwa watoto,wasichana,wanawake wajawazito na wanaonyonyesha kwa kamati za lishe za Halmashauri tarehe 28 Agosti, 2017.

Aidha Bibi Pendo ameendelea kusema hatutegemei Kwimba kuzungumzia masuala ya utapiamlo

“Ni swala la aibu kuzungumzia maswala ya utapiamloa wakati Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ina  vyakula vya aina mbalimbali na inaongoza kwa kuwa na ng’ombe wengi katika mkoa wa Mwanza”

Ni azma ya serikali kutokomeza utapiamlo ili kupata kizazi kitakachotupeleka kwenye Tanzania ya Viwanda. Hayo yamesemwa na DKT Laurent Mselle kutoka Taasisi ya Chakula Lishe Tanzania wakati  akieleza malengo ya Mkutano wa Uhamasishaji kuhusu maswala ya Lishe kwa watoto,wasichana,wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.

Naye Bibi Abela Twin’omujuni kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania amesema tuwahimize wanawake wajawazito wajifungulie kwenye vituo vya afya ili waweze kupata elimu ya uzazi na kupunguza idadi ya akina mama wenye upungufu wa damu na uzito.



Bibi Abela Twin'omujuni kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akielezea  umuhimu wa wanawake wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya Afya .


Akizungumza katika ufunguzi huo Bibi Mary Victor Kibona amehimiza masula ya lishe kwa watoto wachanga na wadogo

“Mtoto anyonye maziwa ya mama pekee na asipewe chakula chochote hata maji katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo kunyonyesha mtoto kunastawisha uhai, afya na maendeleo yake kiakili hivyo kumsaidia katika maisha ya baadaye,ikiemo elimu”

Hata hivyo aliendelea kuhimiza ulishaji wa vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miezi sita.

“Mtoto wenye umri zaidi ya miezi sita wapate chakula mchanganyiko na chenye madini ya chumvi kwa wingi na waasiishie kulishwa michuzi”



Bibi Mary Kibona kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe akihimiza masuala ya lishe kwa watoto wachanga na wadogo

Kwa kuhitimisha  ufunguzi huo Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi  Ngd.Jafari Magesa amesema ni lazima Halmashauri zielimishe jamii umuhimu wa matumizi ya vidonge vya kuongeza damu,kutoa na kusimamia dira ya serikali katika jamii na kuhahakikisha malengo ya huduma yanafikiwa kwa kushirikiana na wadau wengine kufikia nchi ya viwanda.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.