• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

KAMATI YA SIASA WILAYA YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 44 YA CCM.

Posted on: February 5th, 2021

Katika kuadhimisha miaka 44 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kamati ya Siasa ya WIlaya ya Kwimba imefanya ziara ya siku mbili (3-4/02/2021) kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa,Katika ziara hiyo kamati imekagua na kupongeza juhudi zinazoonyeshwa na Halmashauri katika kuhakikisha miradi inakamilika na kamati imeshauri miradi isimamiwe kwa ufasaha na utekelezaji uzingatie muda uliokusudiwa na Wizara.Pongezi hizo zimetolewa na Ndug. Anatori Nshange Katibu wa Chama kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama.


Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni miradi ya Elimu ikwemo ujenzi wa vyoo vya kisasa Shule ya msingi Kadashi,ujenzi wa Chuo cha VETA Ngudu na  ujenzi wa bweni,vyoo na madarasa mawili shule ya sekondari Tallo, hapo kamati ilipongeza uongozi wa shule ya Tallo kwa usimamizi mzuri wa miradi iliyokamilika na inayoendelea kujengwa vilevile wajumbe wa kamati wameshauri kwa kuwa majengo yameboreshwa na taaluma iboreshwe kwa maana ya matokea kwa kidato ya pili,nne na sita.

Majengo ya chuo VETA


Vyoo vya Shule ya Msingi Kadashi

Bweni Tallo Sekondari


Kamati imetembelea miradi ya Afya, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo majengo manne yaani jengo la wagonjwa wa nje (OPD),Maabara,Utawa na jengo la mionzi vinaendelea kukamilishwa,pia wametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya Kadashi ambapo mpaka sasa kuna majengo matatu jengo la wagonjwa wa nje,Maabara na jengo la Mama na Mtoto(jengo la wazazi), hapo  kamati imeshauri kasi ya ujenzi wa kituo hicho iongezwe kwani wananchi wanahitaji kupata huduma kwenye Kituo hicho ili waepuke kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya.

Jengo la OPD la Hospitali ya Wilaya

Jengo la wazazi Kituo cha Afya Kadashi


Vilevile kamati ilitembelea miradi ya maji ya Isunga-kadashi ambapo mradi ulishakamilika kwa zaidi ya  asilimia 80 na wananchi wananufaika na mradi huo,pia mradi wa maji wa Shirima-Izizimba -Mhande hapo kamati iliwataka MWAUWASA kukamirisha mradi huo kwani wananchi wa maeneo hayo wanataabika kutafuta maji maeneo ya mbali vilevile walishauri ufumbuzi wa haraka ufanyike ili vifaa vilivyokosekana vya kumalizia mradi huo vipatikane na mradi ukamilike.

Tanki la maji Izizimba A

Tanki la maji Ngudu

Kliniki ya Mifugo 


Kamati hiyo imekagua barabara za rami zenye urefu wa kilometa 1.2 na kushauri barabara hizo zitengenezwe baadhi ya maeneo yaliyobaki ili zikabidhiwe, na kamati imeshauri Kliniki ya Mifugo ianze kufanya kazi za kiushauri wakati vifaa vya kliniki vikisubiliwa.Wajumbe wakamati hiyo wamesisitiza kuwa Kantini ya Halmashauri ikamilike ili ianze kutumika na kuiongezea Halmashauri mapato.Aidha Katibu wa Chama amesisitiza kuwa kamati hiyo inachotaka kukiona ni utekelezaji wa Ilani ya CCM hivyo miradi yote inapaswa kukamilika ili malengo ya Chama yatimie.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.