• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

KAMATI YA SIASA YA MKOA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: March 18th, 2022

"Hela za miradi tuziogope kama hela za sanda" haya yamesemwa na Mwenezi wa Chama cha  Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Mhe.Simon Mangelepa kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza ambapo alikuwa akimuwakirisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa.


Akiongea katika ziara hiyo Mheshimiwa Mangelepa  amewataka watu wote wanaosimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuogopa fedha hizo na wasimamie miradi kwa weredi ili malengo ya Mheshimiwa Rais yakamilike kama ilivyokusudiwa.


Aidha Mwenezi amempongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha za kuanzisha Shule mpya za Sekondari kitu kitakacho hamasisha watoto wengi kuendelea na masomo ya Sekondari kwani maeneo yanayojengwa Shule mpya yatawapunguzia umbali wa kutembea kwenda Shuleni,Mwenezi amewasisitiza Wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo kwani miradi niyakwao


"simamieni, mshiriki ili kuhakikisha miradi inakamilika kama ilivyokusudiwa msiwaachie viongozi tu, hii miradi niyakwenu" amesema Mangelepa


Katika Ziara hiyo miradi iliyokaguliwa ni Ujenzi wa kituo cha Afya Isunga ambacho kilipokea milion 250 kwaajili ya kuanzisha majengo matatu ambapo limejengwa jengo la Wagonjwa wa nje(OPD), Maabara na kichomea taka. Mradi mwingine ni usambazaji wa umeme katika vijiji 55 vilivyokuwa bado havijapata huduma hiyo, ujenzi wa Daraja mradi uliotekelezwa chini ya TARURA, ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nkalalo ambapo miloni 470 zimeshapokelewa na ujenzi unaendelea, ujenzi wa Chuo cha VETA  ambapo walipokea bilion 1.6 ya kuanzisha Chuo na sasa wamepokea milion 500 ya kukamilisha chuo hicho,na ukarabati wa Chuo cha Afya Ngudu ambapo  walipokea milion 419.5 ili kufanya ukarabati ambapo tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho mwaka 1978 kilikuwa hakijawahi kufanyiwa ukarabati.


Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi Kwimba, pia ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi kwa nguvu zao pale inapobidi na kwaulinzi amewataka Wananchi kutofumbia macho hali yoyote itakayoashiria kukwamisha miradi inayotekelezwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.