Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija akiwa na kamati ya Usalama wakizungumza na Mkurugenzi wa KASHUWASA Eng Patrick Nzumba wakijadili mikakati ya kuhakikisha maji yanapatika kwa wingi Kata ya Ngudu.
Ngudu ni kata pekee hapa Wilayani Kwimba inayohudumiwa na MWAUWASA ambapo chanzo cha maji ya Ngudu ni kutoka kwenye chanzo cha maji cha Shinyanga KASHUWASA.
Chanzo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea upatikanaji wa maji kupungua, hivyo viongozi hao wamekutana jana tarehe 2.10.2024 kujadiliana namna ya kutatua changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha za kubadirisha miundombinu ya mabomba yanayotumika ambayo yanapasuka marakwamara kwa sababu ya Uchakavu.
" changamoto kubwa ni uchakavu wa bomba kubwa linalotokea Kijiji cha Mhalo kuja huku Ngudu ni bomba la mwaka 1974 kwahiyo linapasuka marakwamara" alisema Mkurugenzi huyo wa KASHUWASA
Aidha viongozi hao wamepanga mikakati ya kufufua visima ili kuongeza upatikanaji wa maji " tushirikiane kuhakikisha tunapata fedha za kufufua visima ili tuongeze upatikanaji wa maji na tuwaepushe Wananchi na magonjwa ya milipuko, kama kipindupindu" alisema Ludigija
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.