KAMATI YA USALAMA YAFANYA ZIARA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Posted on: December 10th, 2024
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija akiwa ameambata na kamati ya usalama wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi.
Ziara hiyo imefanyika leo 10,Desemba 2024 ambapo miradi mbalimbali imekaguliwa ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Sekondari Bumyengeja ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Kamati hiyo Imekagua ujenzi wa mabweni katika Shule ya sekondari Sumve, ujenzi wa madalasa shule ya msingi Samilunga na Mhulya na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika kata ya Malya.
Aidha kamati hiyo imekagua ukamilishaji wa Kituo cha afya Isunga ambapo Mheshimiwa Ludigija amewataka wasimamizi kukamilisha kituo hicho kabla ya Januari 2025, Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa vituo vilivyoanza kujengwa pamoja na kituo hicho vilishakamilika na vinatoa huduma lakini kituo cha Isunga bado kinasuasua
" naelekeza kuwa kabla ya Januari hiki kituo kikamilike na fedha zilizoletwa kukamilishe zitumike na kutosheleza kila kitu sitaki kusikia fedha hazitoshi wakati wengine wamejenga kwa milion 500 na zimetosha nyie mmeongezewa fedha na bado mnasuasua" amesema
Akikagua miradi ya Elimu Mheshimiwa Ludigija ametoa wiki mbili kuhakikisha miradi ya ujenzi wa madarasa inakamilika kabla ya tarehe 25 Desemba ili shule zitakapofinguliwa wanafunzi waweze kutumia madarasa hayo.
Kamati hiyo imekagua miradi inayotekelezwa katika Jimbo la Sumve na ziara hiyo itaendelea kesho ambapo miradi inayotekelezwa katika Jimbo la Kwimba itakaguliwa.