• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ahaidi Miundombinu Rafiki Kwa Watu Wenye Ulemavu

Posted on: October 23rd, 2017

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndg Andrea Ng’hwani kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kwimba ameahidi kabla ya Mwaka Fedha 2017/2018 kuisha ataakikisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ina miundombinu rafiki kwa watu wenye Ulemavu.

Ndg Andrea Ng’hwani aliyasema hayo wakati wa kikao  cha kutoa mrejesho wa Mchakato wa Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Rasilimali na Matumizi ya Fedha za Umma kwa watu wenye Ulemavu kupitia Mradi wa “Zijue Haki zako  Mtu Mwenye Ulemavu kupitia Sera ya Afya ya 2017”  kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama cha Walemavu  tarehe 24 Octoba, 2017.

Akiwasilisha mada juu ya  ufuatiliaj wa Mgawanyo na Matumizi ya Rasilimali za Umma katika sekta za Afya, Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali MNGON (Umoja wa NGO’S katika mkoa wa Mwanza) Ndg Adam Ndokeji aliishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata na Vijiji kwa ushirikiano waliouonyesha  katika upatikanaji wa taarifa muhimu  za Watu wenye Ulemavu.




Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali MNGON (Umoja wa NGO’S katika mkoa wa Mwanza) Ndg Adam Ndokeji akisoma Taarifa za Ufuatiliaji wa Mgawanyo na Matumizi ya Rasililmali za Umma katika Sekta ya Afya

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Ndg Vicent Bushaija kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji alikipongeza  Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo Wilayani Kwimba kwa namna kinavyofanya kazi zake kwa bidii na kuishirikisha Serikali. Aliendelea kusema Halmashauri kwa upande wake itaendelea kutekeleza Sera ya Watu Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 ili kuhakikisha maslai ya Watu Wenye walemavu yanazingatiwa.

Aidha aliwataka watu wenye Ulemavu kutumia fursa mbalimbali zikiwemo za Mikopo inayotolewa na Halmashauri ili kuanzisha na kuendesha Miradi ya Kiuchumi ili kukuza kipato chao.



Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Ndg Vicent Bushaija akiongea na washiriki wa kikao cha Mrejesho wa Matokeo ya Utekelezaji wa Shuguli za Mradi wa“Zijue Haki zako  Mtu Mwenye Ulemavu kupitia Sera ya Afya ya 2017”.

Katibu wa CHAWATA Wilayani Kwimba  Ndg Andrew Sabuni alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kuwa Watu Wenye Ulemavu wa Viungo wawe wanahusishwa kwenye kamati mbalimbali za maamuzi kuanzia ngazi za vijiji hadi Halmashauri.



Mwenyekiti wa chama Chama cha Walemavu Wilayani Kwimba Ndg Nyerere Julias Musa akichangia taarifa wakati wa kikao cha kutoa Mrejesho wa mchakato wa Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Matumizi ya Fedha za Umma kwa Watu Wenye Ulemavu (PETS).


Imam wa Msikiti wa Ngudu Ndg Nassor Husein Mokiwa alisema kwa kupitia Mradi wa Zijue Haki za Mtu Mwenye Ulemavu waumini wa dini ya kiislamu wamehamisika kutengeneza Miundombinu  rafiki kwa Watu Wenye Ulemavu katika Msikiti wa Ngudu Mjini ili kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili Watu Wenye Ulemavu wakati wakuingia na kutoka Msikitini.

Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Wilayani Kwimba Ndg Nyerere Julias Musa aliiomba Serikali kupunguza Riba kwa mikopo inayotolewa  kwa Watu Wenye Ulemavu ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

 Mradi wa “Zijue Haki zako  Mtu Mwenye Ulemavu kupitia Sera ya Afya ya 2017”  Wilayani Kwimba  Umetekelezwa katika kata ya Ngudu, Fukalo, Igongwa na Nkalalo  ambapo wanufaika wa moja kwa moja  ni walemavu 72 kati ya wanaume 32 wanawake 40 na wanufaika wasio wa moja kwa moja ni jamii  wanaume wakiwa 370 na wanawake 227 jumla ni 597 waliofikiwa na elimu ya Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Rasilimali na Matumizi ya Fedha za Umma kwa watu wenye Ulemavu.


Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.