Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendeleo kuenzi fikra za Rais wa awamu ya kwanza Hayati Mwalimu JK Nyerere katika kupambana na ujinga , maradhi na umasikini. Ili kuhakikisha haya yanafanikiwa Halmashauti imekuwa ikiweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya Elimu na Afya ili kutokomeza ujinga na kuwahakikishia Wananchi upatikanaji wa huduma bora za Afya.
Katika kutekeleza hilo miundombinu ya Shule inaendelea kuboreshwa, na miundo mbinu ya Vituo vya kutolea huduma za Afya inaboreshwa katika kata zote za Wilaya ya Kwimba.
Kupinga umaskini imekuwa ni agenda ya kudumu katika Halmashauri ya Kwimba, katika kufanikisha hilo mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani imeendelea kutolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili kuhakikisha vijana wanafanya kazi za kuwaongezea kipato na kujikomboa na umasikini.
Baba wa Taifa tutaendelea kuenzi fikra zako.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.