• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Kwimba Yaadhmisha Siku ya Mtoto wa Afrika

Posted on: June 19th, 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeadhimisha  siku ya mtoto wa Afrika katika kijiji cha Isageng’he kata ya Mwakilyambiti tarehe 16/06/2017 Kauli mbiu ikiwa “Maendeleo Endelevu 2030 Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa watoto”  lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbuka watoto wenzetu waliouawa na utawala  dharimu wa makaburu wa Afrika ya kusini tarehe 16.06.1976, katika kitongoji cha Soweto.

 Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya kwimba Ndg Joseph Mwikwabe ambaye ni Afisa Tarafa ya Nyamilama amewaomba wazazi/walezi wa watoto na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto wote bila ubaguzi.

“Tunapambana vikali ili kutokomeza kabisa ubaguzi wa watoto katika kupatiwa elimu kikamilifu na ndoa za utotoni kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaohusika kuoa au kuwapa mimba wasichana wadogo”.

Ndg Joseph pia ameagiza kuwa viongozi wote katika vitongoji,vijiji, kata na wilaya wahakikishe amani inakuwepo miongoni mwa watoto na wazazi/walezi ili kudhibiti mimba kwa wasichana   kitu ambacho inabidi  tukikemee kwa nguvu zetu zote. Hii ni pamoja na kuweka/kuwepo miundo mbinu rafiki shuleni na hasa kwa watoto wenye ulemavu na wanafunzi wote kwa ujumla.

Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mtoto Salumu Jonas Lutaja kwa niaba  ya watoto wa wilaya ya kwimba ameiomba jamii kutekeleza Haki za Msingi za Watoto ikiwa ni pamoja na Haki ya kuishi, Haki ya kulindwa, Haki ya  kupata elimu bora na Haki ya kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Ndg Joseph kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ametoa Zawadi ya Vyandarua kwa akina mama watano (05) wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano ambao walikuwa wanaoudhuria cliniki vizuri ili ziweze kuwasaidia na kuwakinga  watoto hao na ugonjwa wa Malaria.

Aidha Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Ngudu Bibi Elizabeth Lucas amewafungulia watoto hao watano  akaunti ya watoto “Junior Jumbo Account” katika bank  ya CRDB Tawi Ngudu na kwa gharama ya shilling elfu tano tano kila mmoja.

Kwa kuhitimisha sherehe hizo Ndg Joseph ametoa shukrani zake kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi vya kijamii na wadau wote kwa jitihada zao za kuwasaidia watoto walio katika mazingira hatarishi. Mchango wao tunauthamini na tunaomba tuzidi kushirikiana  katika maeneo mbalimbali ya wilaya yetu ili tuweze kusaidia watoto wengi zaidi.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.