KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU
Posted on: February 21st, 2025
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeendelea kuviwezesha vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani.
Jumla ya milioni 607 zimetolewa leo Feb. 21,2025 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambao wameaswa kwenda kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
" wito wangu kwenu nendeni mkafanye kazi mlizoandika kwenye maandiko yenu ili mkaweze kuzarisha fedha hizo na muweze kujiinua kiuchumi, pia niwasisitize tu kwamba fedha hizo hazina riba lakini zinarejeshwa kwahiyo marejesho ni lazima" amesema Ludigija
Akiongea na vikundi hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo amewataka watu wote waliopata mkopo huo kuwa na nidhamu ya fedha ili waweze kutimiza malengo yao
" hakikisheni mnakuwa na nidhamu ya fedha siyo umepewa mkopo kwaajili ya biashara wewe unaenda kutumia fedha hiyo kuoa, mkifanya hivyo mtashindwa kurejesha harafu mtaanza kukamatwa na kupelekwa polisi, niwasisitize kafanyeni kazi kurejesha ni lazima ili na wengine wapate" Ludigija
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt Amon Mkoga amewataka wanavikundi waliopata mikopo kwenda kuendeleza miradi na kutafuta fursa za biashara maeneo mbalimbali " ombeni kufanya biashara na Halmashauri kwamfano mnaopika chakula na kazi nyingine" amesema Mkoga
Wanavikundi waliopokea mikopo hiyo wamemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikopo hiyo ikuanza kutolewa na wameahidi kwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.