• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Kwimba Yaweka Mkakati wa Kudhibiti Utoro Mashuleni

Posted on: April 21st, 2017


Watendaji wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba wametakiwa kuhakikisha wanasaidia kukomesha  tabia za utoro shuleni. Wanafunzi wanaoandikishwa shule sharti wamalize shule na wanakuwapo Shuleni kila siku za shule, watoro wote wapewe adhabu kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu za shule.

 Wito huo umetolewa na  Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza ndugu, Juma Kasandiko wakati wa kikao cha Mpango mkakati wa kuinua Taaluma  Mkoa wa Mwanza kilichofanyika  wilayani Kwimba katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu na baadaye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Nella. Kikao hicho kiliwashirikisha Wakuu wa Shule,Walimu Wakuu, Watendaji wa Kata, Waratibu Elimu Kata na Walimu wa Taaluma.

Katika kikao hicho Ndugu Juma Kasandiko  aliwataka Walimu kujisomea zaidi ya vitabu vitatu ili wawe na maarifa ya kutosha  na kutumia njia shirikishi  wakati wa ufundishaji na ujifunzaji. Pia amewakumbusha wakuu wa shule kuteua wakuu wa Idara za Masomo wenye maarifa ya kutosha katika masomo hayo.  “Suala hili litatufanya kufikia mpango mkakati tuliojiwekea wa kupata daraja la kwanza kwa asilimia 50 la pili  asilimia 40 na la tatu asilimia 10”, alisisitiza.

Aliendelea kumpongeza Mkuu wa Shule wa Shule ya Sekondari Mwamashimba Bi. Edina Mkama kwa kufaulisha vizuri mtihani wa “MOCK” kidato cha sita mwaka 2017.Katika matokeo hayo, idadi ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi 86, daraja la pili wanafunzi 02 na jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 88.

Afisa Elimu huyo wa Mkoa amewaomba Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu  kuwashirikisha Walimu wao katika shughuli zote zinazofanyika Shuleni ili kuondoa  mpasuko wa wao kwa wao na amewataka kuitisha vikao vya mara kwa mara ili kupeana taarifa mbalimbali juu ya boreshaji wa elimu.

Afisa Elimu Taaluma Sekondari Mkoa wa Mwanza Ndugu,  Joseph Ngoseki aliwaonya Wakuu  wa Shule wenye upendeleo wa kuwapa motisha  walimu  kwani kwa kufanya hivyo ni kuwawakatisha tamaa walimu katika kutimiza wajibu na majukumu yao. “Wakuu wa Shule na Walimu wa Wakuu  hakikisheni mnawapongeza walimu wanaofanya vizuri”.

 Aidha alikemea vitendo viovu vinavyofanywa na Walimu wa kiume kwa kuwakatisha masomo watoto wa kike na ameahidi kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu watakaokutwa na makosa hayo.

Wakatiwa kufunga kikao hiyo Afisa elimu sekondari Bw Lawi Kajanja alimuunga mkono  Bw Joseph  Ngoseki kwa kuwatahadharisha walimu na umma kwa ujumla kuwa ni kosa kisheria kusababisha au kushawishi mwanafunzi kutohudhuria masomo yake kwa namna yoyote ile. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na.25 ya Mwaka 1978 na marekebisho yake ya mwaka 2013 sehemu ya 35, ibara ya 4 (sehemu ndogo ya ii-iii) ya kifungu hicho.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.