• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Kwimba yazindua Rasmi Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi

Posted on: May 10th, 2017

Halmashauri ya wilaya ya Kwimba  imezindua rasmi jukwaa la uwezeshaji Wanawake kiuchumi siku ya tarehe 9\5\2017, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya kwimba. Uanzishwaji  wa jukwaa hili ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hasani likiwa na  lengo la kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli zingine za kiuchumi.

Kaim Afisa Elimu Sekondari  Bw Boniventure Ng’andilo ambaye alikuwa mgeni rasmi  akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba  katika hafla hiyo alitoa  wito kwa wanawake wa Wilaya ya Kwimba kuzitumia vizuri fursa mbalimbali zinazowazunguka katika maeneo wanamoishi ili kujikwamua na hali duni ya maisha kwani anatambua kuwa mwanamke anaweza, jamii iwape nafasi ili waweze kuleta mabadiliko katika masuala mazima ya maendeleo.

Aidha,  Bw Boniventure Ng’andilo amevihasa vikundi vinavyopata mikopo vitumie vizuri mikopo inayopatikana na kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kukopeshwa.

Akitoa maoni yake katika hafla hiyo, Bibi Christina Bunini ambaye pia ni Kaimu Afisa utumishi

wa Wilaya ya Kwimba amewataka wajasiliamali wenzake kuwa na lugha nzuri katika maeneo yao ya  biashara  kwani ni mbinu mojawapo ya kuvutia wateja kwenye biashara.

Naye Bi Happy Kaali, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Ngudu aliongeza kwa kueleza kwamba muda ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo ni vyem ukatumika vizuri katika biashara kwani kwa kufanya hivyo malengo yataweza kufikiwa kwa asilimia nyingi zaidi.

Kwa upande wake, Bi Flaviana Moro ambaye ni Mratibu wa uwezeshaji kiuchumi ametoa  pongezi  za dhati kwa Taasisi zisizo za Kiserikali, asasi za kidini, wadau wa maendeleo, vikundi pamoja na wanawake wajasiliamali kwa kukubali wito wa kuunda jukwaa la Wanawake na amewatakia utekelezaji mwema wa majukumu ya jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Uzinduzi wa jukwaa  hilo  wilayani kwimba umekwenda sambamba na mafunzo ya ujasiliamali kwa ajili ya kuwainua wanawake Kiuchumi.


Atupakisye M. Mwakalembusya

Afisa Habari 

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba


Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.