Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda Amewapongeza waandaaji wa sherehe hizo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija kwakusimamia maandalizi yote ambapo sherehe hizo zimefanyika Kimkoa Wilayani Kwimba leo tarehe 1 Mei,2025
Mkuu huyo ameahidi kwenda kufanyia kazi changamoto zote zilizowasilishwa kwa njia ya mabango na kwenye risala.
"Serikali imefanyia kazi mambo mbalimbali kwa watumishi ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya watumishi,madai ya watumishi kama rikizo,matibabu na watumishi 9829 wamepandishwa madaraja" amesema Mtanda
tunaw0apongeza wafanyakazi wote waliotekeleza majukumu yao vizuri, muendelee kuchapakazi kwa bidii, muwe waadilifu na wenye kutiana moyo katika kuchapa kazi"
Pia amewataka wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo limeanza leo Mei 1, 2025 kwa Mkoa wa Mwanza kwenda kujiandikisha ili wapate haki ya kupiga kura . " uchaguzi umewadia, maandalizi yanaendelea kwahiyo kama hutajitokeza kujiorodhesha utajikosesha haki ya kupiga kura"
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija amewakaribisha wafanyakazi wote wa Mkoa wa Mwanza na kuwapongeza kwa kuendelea kuwa watumishi bora wanaotekeleza majukumu yao kwa weledi.
Wakala wa usalama na afya mahali pa kazi ( OSHA) nao wakatoa rai kwa watumishi kuzingatia usalama na afya " sasa mwaswala ya usalama na afya mahali pa kazi ni jambo la lazima na la msingi" pia amewasisitiza wafanyakazi kuchagua viongozi watakaobeba maono ya Rais ya usalama na afya ambao watachukua jambo hilo kwa uzito.
Akisoma risala katibu wa maandalizi ya sherehe hiyo amemuomba mgeni rasmi kufanyia kazi changamoto mbalimbali ikiwe kutowasilisha michango ya watumishi kwenye mifuko ya jamii jambo linalipelekea usumbufu kwa wastaafu, watumishi kutolipwa fedha za rikizo kwa wakati, pia ametoa wito kwa waajili wasiwahamishe watumishi kama hawajaandaa malipo.
Aidha ameomba mishahara iongezwe kwani hali ya gharama za maisha zinapanda kila siku lakini mishahara iko palepale, na kikokotoo kifanyiwe kaz
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.