" Ndugu wananchi ugonjwa wa UKIMWI umekuwa ni tishio kubwa sana na Serikali imeendelea kufanya juhudu mbalimbali kuzuia ugonjwa huu kusambaa" amesema Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija kwenye maadhimisho ya UKIMWI.
Ugonjwa huu bado haujapata tiba wala chanjo kwahiyo ni muhimu kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huu ili kuepuka athari zinazosababishwa na maambukizi ya ugonjwa huu, alisisitiza
Mhe. Ng'wilabuzu amesema maambukizi ya ugonjwa yameshuka kutoka asilimia 7.2 hadi 4.7 Mwanza lakini bado hiki nikiwango kikubwa cha maambuki hivyo wananchi tuendelee kuchukua tahadhari.
Mhe. Ng'wilabuzu Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amewasisitiza wananchi kutowanyanyapaa watu wanaoishi na virusi
" nitoe rai kwa wazazi na walezi kuongeza juhudi katika kuwahamasisha vijana kujikinga na kutowabagua waathirika"
Amewashauri wananchi kutojificha bali wawe tayari kujitokeza kupata dawa pindi wanapojua wamepata maambukizi ya virus hiyo.
" nitumie nafas hii kuwashukuru waviu kwa kutoa risala inayoonyesha hali halisi ya watu wanaoishi na virus kwa kuendelea kuelimisha watu wengine kujitokeza kupima na kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi.
Akiwasilisha risala ndugu. Julias Mwenyekiti wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Wilaya ya Kwimba amesema idara ya Afya imeendelea kuboresha mapambano dhidi ya ukimwi kwa kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo, kugawa condom kwa wananchi, kuhamasisha wananchi kupima mara kwa mara na huduma nyingine.
Maadhimisho hayo yamepambwa na matukio mbali ikiwa ni pamoja na ngoma za asili, maigizo, nyimbo za kwaya zilizohamasisha wananchi kujikinga na gonjwa la UKIMWI
Katika maadhimisho hayo huduma mbalimbali za afya zimetolewa ikiwa ni pamoja na kupima UKIMWI,kupima kansa ya kizazi, kupima presha, tohara na huduma nyingine.
Aidha wadau wa afya wameshiriki maadhimisho hayo ambapo wameonyesha huduma wanazotoa katika maeneo mbalimbali. Wadau walioshiriki maadhimisho hayo ni iCAP, Kizazi hodari, TAKUKURU na mashirika mengine.
Maashimisho haya yamekuwa na kauli mbiu inayosema " Chagua njia sahihi, tokomeza UKIMWI "
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.