• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YASISITIZA USAWA

Posted on: March 8th, 2023

Maadhimisho ya Siku wa wanawake  kimkoa yamefanyika Wilayani Kwimba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima ameitumia siku hii kuwaasa wananchi kutobagua watoto katika kuwapa Elimu

" Wananchi nazani mmeona hao wanawake wote waliopita na mabango wakiandamana wamesomeshwa na wazazi wao hawakubaguliwa Kwa sababu niwanawake kwahiyo niwashauri muwape kipaumbele watoto wa kike kwenye swala la Elimu" Malima


Mheshimiwa Malima amesisitiza malezi bora Kwa watoto, amekemea ukatili wa kijinsia, kimwili na kiuchumi, amesisitiza wazazi hasa wa kike kujenga mahusiano mazuri na watoto Ili kujua changamoto zote zinazowakabili na kuweza kuzitatua.


Mkuu huyo amekabidhi majiko ya gesi na vifaa vya kujifungulia Kwa wanawake wajawazito kutoka Kata za Kwimba, vifaa hivyo vimetolewa na mashirika mbalimbali yenye lengo la kuboresha maisha ya wanawake wjawazito.Pia amekabidhi taulo za kike Kwa wanafunzi wa kike wa Shule za Sekondari.


Katika maadhimisho hayo ameshiriki  Waziri wa Ardhi Mhe Angelina Mabula na Naibu Waziri wa Maliasil na Utali ambao wamewapongeza wanawake wote walioshiriki maadhimisho huku wakisisitiza malezi bora Kwa watoto wakike na wakiume Ili kuwaepusha na madhara yanayosababishwa na mmomonyoko wa Maadili.


Aidha viongozi hao wamewataka wanawake wote wanaopewa nafasi ya kuongoza  wajiamini na wafanye kazi zao Kwa weledi Ili waunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais za kuwaletea Wananchi maendeleo


"awe kiongozi wa kikundi,awe kiongozi Ofisi za Serikali au taasisi anatakiwa kujiamini Kwa sababu wanawake  wamemuweka pale, tulioko maofisini tupo kwaajili ya kutumikia jamii nzima kwahiyo tuangalie watangulizi wetu pamoja na kuangalia Rais wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anatusababishia kutembea kifua mbele maana miradi ya kimkakati inaendelea,miradi ya Afya, amepunguza riba ya Kodi ya Ardhi haya yote yanafanywa na mwanamke shupavu" amesema Angelina  Mabula


 Siku ya wanawake Duniani  huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi ambapo mwaka huu yamekuwa na kauli mbiu inayosema

"UBUNIFU WA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA, CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA"

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.