Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija amekabidhi pikipiki kumi kwa maafisa ugani kwaajili ya kurahisisha kazi zao za kuwatembelea wakulima na wafugaji kwenda kuwapatia elimu ya kulima na kufuga kisasa
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya amewataka kwenda kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kusaidia kata zote kupata elimu ya kilimo
" tunawakabidhi pikipiki hizi ili mkasaidie kata zote kutoa huduma ya ugani,kubwa zaidi waelimisheni wafugaji waache kufuga kwa mazoea wafuge kisasa" amesema Ludigija
Mkuu huyo amesisitiza kuwa wapo wafugaji ambao walianza kufuga wakiwa vijana hadi wamezeeka sasa wao wanajiona kama wataalamu wa mifugo hao nao waelimishwe ili waepukane na hasara inayowapata mifugo inapopatwa na magonjwa
Katika hafla hiyo ameshiriki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt.Amon Mkoga ambaye amewataka Maafisa uganii wote waliopata vyombo hivyo kwenda kuvitumia vizuri na kuvitunza ili vidumu na viwarahisishie kazi
" nitumie fulsa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia pikipiki hizi ili zitusaidie kusimamia shughuli za kilimo na mifugo na kama mnavyojua mapato yetu yanategemea kilimo na mifugo kwa hiyo mwende mkazitumie vizuri hizi pikipiki ili zidumu" amesema Mkoga
Naye Afisa Mifugo Ndugu Beatus Mashinji amesema jumla ya pikipiki 17 zimekabidhiwa kwa maafisa ugani ambapo pikipiki saba zilikabidhiwa awali na pikipiki kumi zimekabidhi leo, " kupatika kwa pikipiki hizi kunaenda kurahisisha kazi ya ugani maana maafisa wanatakiwa wawatembelee wakulima na wafugaji ili kuwapatia elimu kwahiyo hivi vyombo vitarahisisha kazi"
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea kuboresha sekta ya kilimo na mifugo ili kuongeza tija kwa wakulima na kuongeza upatikanaji wa mapato.