Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imefanya Mkutano wa baraza la Madiwani robo ya Kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 siku ya kwanza jana Novemba 12,2024 ambapo taarifa za Kata na taarifa za taasisi zilipo Wilayani Kwimba zimewasilishwa huku waheshimiwa madiwani wakimtaka Meneja wa TARURA kuhakikisha barabara zilizo haribiwa na mvua zinakarabatiwa
" barabara zimeharibika sana na mvua ndio zimeanza saizi na kuna maeneo mengine makalavati yameharibi na yanasababisha ajari kwa wananchi hizi barabara zikarabatiwe" amesema Mhe. Shinje Deusi
Waheshimiwa madiwani wamemtaka meneja wa Tanesco kuhakikisha umeme unafika kwenye taasisi zote za Umma huku msisitizo ukiwa umeme wa kila kitongoji uzingatie kila kata
" tulipata taarifa kuwa umeme kila kitongoji Wilaya ya Kwimba tulipata vitongoji 30 kwahiyo tunaomba mgawanyo uzingatie kila jimbo na kila kata" amesema Mhe. Peter Msalaba
Aidha wameshauri miradi ya maji ambayo imetekelezwa kwa muda mrefu na haijakamilika wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo wachukuliwe hatua
Katika kikao hicho Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt.Zuber Mzige ametoa taarifa ya hari ya kipindupindu huku akisisitiza ushirikiano kwenye kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa huo
" kipindupindu kinasababishwa na uchafu, hivyo tunawaomba mnapokuwa na mikutano au mikusanyiko waambieni wananchi umuhimu wa kuzingatia usafi,kuchemsha maji ya kunywa na kunawa,kujenga vyoo na tutaanza kukagua vyoo tutakayemkuta hana choo tutamtoza faini" amesema Mzige
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt Amon Mkoga amesisitiza kuwa elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili kuondoa maambukizi ya kipindupindu.
Akiahirisha Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Thereza Lusangija amewataka wajumbe wa mkutano huo kwenda kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.