Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wamemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali Kwimba kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo.
Wameyasema hayo leo Agosti 29,2024 kwenye Mkutano maalumu wa kufunga hesabu za Halmashauri ambapo imebainika kuwa hesabu za mwaka wa fedha 2023/24 zimefungwa Halmashauri ikiwa na fedha taslimu shilingi bilioni 8.26
" tunaipongeza Serikali kwa kuendelea kuijali kwimba kwasababu fedha za miradi zinaendelea kuletwa hili ni jambo la kufurahisha kufunga mwaka Halmashauri ikiwa na bilioni 8" amesema Mhe. Athanas Nigo Diwani Kata ya Malya
Akiwasilisha taarifa ya hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2023/24 Ndugu Kassim Shomvi Kaimu Muweka Hazina (W) Kwimba amesema Halmashauri imefunga mwaka ikiwa na fedha taslimu shilingi bilioni 8.269 zikiwa ni fedha za miradi,mali za kudumu zenye thamani ya shilingi bilioni 76.89, pia amesisitiza kuwa Halmashauri inaendelea kulipa madeni kwani zaidi ya milioni 300 zimelipwa kwenye mwaka wa fedha 2023/24.
Akifunga mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Lameck Hole amesema Halmashauri inaouwezo wa kujiendesha kwani inazo Mali za kudumu zenye dhamani ya shilingi bilioni 76.8 pia inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.