• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

MADIWANI WANG'AKA WATAKA WADAIWA SUGU FEDHA ZA MIKOPO 10% KUKAMATWA

Posted on: December 15th, 2022

Wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Kwimba( DCC) wameshauri wadaiwa sugu wa madeni ya mikopo ya vikundi vinavyokopeshwa na Halmashauri wakamatwe na jeshi la police kama hawataki kilipa fedha hizo kwa hiari.

“ wadaiwa wakamatwe warudishe fedha ili watu wengine wakopeshwe, tena hiki kikosi kazi kilichoanza kuwakamata  kiongeze nguvu  zaidi na wanapokamata wasibague, watu wote wanaodaiwa wakamatwe walipe, hatuwezi kubembeleza watu kurudisha fedha wakati walisaini mikataba ya kurudisha fedha hizo ndani ya mwaka mmoja” amesema Majoge Diwani Hungumalwa 

Haya yamejiri kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (  DCC ) ambacho kimefanyika leo tarehe 15, Disemba 2022 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi ameshauri vikundi vinavyokopeshwa virudishe fedha hizo kwa wakati  wasisubiri hadi wakamatwe ndipo warejeshe

“ dawa ya deni ni kulipa, wanaodaiwa walipe fedha wasisubir kukamatwa, lakini kuhusu elimu vikundi vinapewa elimu kabla ya kukopeshwa  kwahiyo kutorejesha ni tabia ambayo vikundi  vingi wanafikiri fedha ya Serikali  haina mtu wa kuifatilia” amesema Samizi

Aidha Mkuu huyo ameshauri Idara ya maendeleo ya jamii ibadirishe utaratibu wa kutoa mikopo kutoka kutoa fedha hadi kutoa vifaa au vitu ili kuepusha tabia ya baadhi ya vikundi vinavyokopeshwa fedha  kisha kubadili matumizi ya fedha hizo badara ya kufanya biashara wanagawana fedha kitu kinachopelekea  kushindwa kurejesha fedha hizo.

Nao wafugaji wametakiwa kuacha tabia ya kupitisha mifugo barabarani hali inayosababisha  uharibifu wa barabara

“ kamateni mifugo yote  inayopita barabarani muwatoze faini ya elfu 50 kila ngombe ili iwe fundisho kwa wafugaji wote wasiotaka kufuata sheria na taratibu za Serikali” amesema Samizi

Katika Kikao hicho taarifa za taasis mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo taarifa za  RUWASA,TANESCO,TARURA,MWAUWASA,VETA, FDC MALYA NA CHUO CHA AFYA NGUDU.









Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.