Waheshimiwa Madiwani wameaswa kuviishi viapo vya uadilifu na uwajibikaji ili kutimiza malengo ya kuwatumikia Wananchi.
Haya yamejiri kwenye Baraza la Kwanza la Madiwani lililofanyika leo 3,Desemba 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri amechaguluwa na kushinda kwa kura 42 kati ya 43
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba ndugu Mohamed Ngasinda Katibu Tawala amewapongeza Madiwani wote kwa kuaminiwa na Wananchi na amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kuaminiwa na Madiwani kusimamia Halmashauri, pia amewataka kwenda kufanya kazi kwa uaminifu,weledi na kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo
" mmesikia tulikotoka na tunakotakiwa kwenda hii kazi mkaifanye Waheshimiwa Madiwani tunataka mwaka huu tuvuke lengo kama tulivyovuka lengo mwaka jana" amesema Ngasinda
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhe.Lameck Hole baada ya kujitwalia ushindi wa kishindo amewaomba Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu wote kufanya kazi kwa ushirikiano huku akiahidi kwenda kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha Halmashauri inafikia malengo yaliyokusudiwa
Katika baraza hilo wameshiriki Wabunge wa Majimbo ya Kwimba na Sumve ambao wamewataka watumishi kwenda kutekeleza majukumu yao ili matokeo yaonekane " sisi tumetumwa na wananchi kuja kuwasimamia watumishi, sisi hatuna mchezo kwenye kazi, tumeahidi mambo mengi kwahiyo tutawasimamia kuhakikisha shughuli zinatekelezwa na matokeo yanaonekana" amesema Mhe. Cosmas Bulala Mbunge Jimbo la Kwimba
Akiwasilisha taarifa ya Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt.Amon Mkoga ameomba ushirikiano ili kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka kuvuka au kufikia lengo ambapo Halmashauri inalengo la kukusanya zaidi ya bilioni nne
" tushirikiane, kwenye jambo lolote la maendeleo tushaurini ili tuweze kufikia malengo ya kuwafikia wananchi kwa kuchagiza maendeleo" amesema Mkoga
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Mhe. Sabana Lushu amewataka Wabunge na Madiwani kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano na watumishi bila kutengenezeana ajari ili wote watimize malengo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.